Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Suleiman Kissoki amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari , Katibu Mkuu wa Shiwata, Michael Kagondela amesema hadi jana jioni, Kissoki alikuwa ofisini Ilala Bungoni akiendelea na majukumu yake.

Kagondela amesema  marehemu huyo amezikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam saa 10 jioni ambako wadau mbalimbali wakiwemo wasanii, wanamichezo  na wengineo walijitokeza kumsindikiza.

Kaka wa marehemu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA), Mussa Kissoki amesema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu kazi yake haina makosa.

Amesema kuwa kama binaadamu yatupasa tujiandae kwa ajili ya kifo kwa sababu hatujui siku wala saa mauti yatakapotufika.

Mbali ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Shiwata, marehemu ametumikia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...