Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imeelezwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakipangisha nyumba na kisha kugeuza kama maghala ya kuficha dawa hizo ,hivyo imewataka wamiliki wa nyumba kuwa makini na watu wanaowapangisha.

Akizingumza leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo alipokuwa akitoa taarifa ya kukamata dawa za kulevya zaidi ya kilo 2,207 katika Mkoa wa Dar es Salaam na Tanga amesema kuna wafanyabiashara wa dawa hizo wanapangisha nyumba lakini hawaishi zaidi ya kuhifadhi dawa za kulevya.

"Mamlaka inatoa rai kwa wamiliki wa nyumba kuwa makini wanapopangisha nyuma zao kwani nyumba inayotumika kwa shughuli za dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na inaweza kutaifishwa.

"Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya sura ya 95 imeweka katazo kwa mmiliki au msimamizi wa nyumba,msimamzi wa eneo au chombo cha usafirishaji kuruhusu vitumike kwa lengo la kutengeneza ,kuvuta,kujidunga ,kuuza au kununua dawa za kulevya,"amesema Kamishina Jenerali Lyimo.

Aidha amesema mmiliki anapojua kuwa kosa linatendeka kwenye eneo lake analojukumu la kutoa taarifa kwa Mamlaka.Kushindwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na akitiwa hatiani adhabu yake inaweza kuwa faini kuanzia Sh.milioni tano hadi Sh.milioni  50 au kifungo cha miaka mitano hadi 30 jela au vyote kwa pamoja.

Amesema kuwa hata katika operesheni ambayo wanaendelea kuifanya ya kusaka wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya Kuna watuhumiwa wamepanga nyumba Kigamboni lakini wenyewe wanaishi Mabibo na hivyo nyumba waliyopangisha inatumika kuficha tu dawa.

Amefafanua kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambao wanapangisha nyumba hizo wamekuwa na usiri kiasi hata mlinzi anaweza kuwa analinda nyumba lakini haijui inatumiwa kuficha dawa za kulevya.

Hata hivyo amesema Mamlaka inatoa shukrani kwa wananchi wanaotoa ushirikiano kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na wanahimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...