Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Paul Sangawe ameongoza Kikao cha Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), wakurugenzi wa sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na timu ya wataalamu.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho pia  kimehusu mapitio ya Mipango na Bajeti ya Programu kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji iliyobakia.

Kikao  hicho kimefanyika tarehe 18 Novemba 2024 Zanzibar, katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...