Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi amefungua Mkutano wa 56 wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji wa utoaji huduma viwanjani kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara.

Akitoa neno la ufunguzi katika Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Bw. Msangi amesema Kamati hiyo inajukumu la msingi la kuhakikisha ina andaa mapendekezo na kutoa maazimo yatakayosababisha utolewaji wa huduma za kasi katika viwanja vya ndege nchini bila kuathiri ufanisi katika masuala ya kiusalama.

Mbali na ufunguzi wa Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA pia alizindua kanuni inayosimamia Uwezeshaji wa utaoji huduma viwanjani.

Awali akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema kuwa mwaka huu Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) linaadhimisha miaka 75 ya Uwezeshaji wa utaoji huduma viwanjani likiwa na kauli mbiu "Past, Present, Future: 75 Years of Enabling Air Travel".

"Katika kuadhimisha miaka hii 75 ya Uwezeshaji na Urahisishaji wa Usafiri wa Anga, tunaowajibu wa kuwa kichocheo cha huduma bora, stahiki na zinazozingatia uharaka na kwa usalama". alisema Bw. Malanga

Mkutano huo wa siku tatu unafanyika kuanzia Novemba 12, 2024 ukiwa na mambo kadhaa ikiwemo ziara ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato ambapo wajumbe wamepata fursa ya kujionea na kupata maelezo juu ya hatua za ujenzi unaoendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akifungua Mkutano wa 56 wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji wa utoaji huduma viwanjani kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA Bw. Daniel Malanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji wa utoaji huduma viwanjani akizungumza wakati  mkutano wa 56 wa Kamati hiyo  unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi aliyemwakilisha  Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara akiwa kwenye picha ya pamoja na  Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji wa utoaji huduma viwanjani wakati  mkutano wa 56 wa Kamati hiyo  unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...