NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya Mapinduzi, Zanzibar kimefadhili wanafunzi 200 kujiunga na Chuo Cha Ufundi Furahika ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchukua mbalimbali zinazofundishwa chuoni hapo.
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya, watasoma kozi ushonaji, hoteli, ususi, upambambaji, makeup na nyinginezo kwa lengo la kuweza kujiajiri ama kuajiliwa pindi watakapohitimu mafunzo hayo.
Mkuu huyo wa Chuo hicho amebainisha leo, Novemba 11, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kufafanua kuwa sasa chuo hicho kinawafunzi zaidi ya 400 wengine wakitokea Tanzania Bara wakiwa wanasoma kozi mbalimbali chuoni hapo.
“Kwa kipekee namshukuru sana na kumpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Hussein Alli Mwinyi na Serikali yake kwa ujumla kwa kuthamini vijana waliotoka katika mazingira magumu na kuwaleta hapa ili wapate elimu itakayowezesha kujikwamua kichumi na kuachana na utegemezi kutoka kwa wazazi ama walezi wao,” amasema.
Ameongeza kwamba wanachotakiwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kutoingusha Serikali ambayo imejitolea kuwafadhili ili wafikie malengo yao katika elimu na kupatia ujuzi utakaowafaa maishani.
“Hizi fedha ambazo Rais Dkt Mwinyi amezotoa kwa ajili ya kuwafadhili wanafunzi hawa zingeweza kwenda kufanya shughuli nyingine lakini amezitoa kwao ili waweze kujikwamua kielimu na kuweza kujitegemea, wanachotakiwa ni kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao ambazo zilionekana kuanza kupotea,” amesema.
Pia Dkt Msuya hakusita kumpongeza Mkurugenzi wa Maendeleo ya jamii, Zanzibar kwa kuonesha ushirikiano na chuo hicho na kuhakikisha vijana wanapata ujuzi na kujitegemea.
Toafuti na hilo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukiamini chuo hicho na kufungua milango kwa vijana ambao ndoto za kuendelea na elimu zilishatoweka ila kupitia chuo hicho wamepata tumaini jipya katika maisha yao.
Kwa upande mwingine, Dkt Msuya ametoa wito wa wazazi na walezi kupeleka vijana wao katika chuo hicho ili kupata ujuzi bure kupitia fani wazitakazo ikiwemo udereva, umeme na nyinginezo bure na tayari dirisha la usajili lipo wazi.
“Niwaombe wazazi na walezi pasipo kujali itikadi ya dini wala siasa wawalete watoto wapate ujuzi hapa elimu ni bure na tunakozi nyingi ambazo mtoto akitoka hapa ataweza kujiajili na kuajilika”,amesema.
Aidha ameongeza kuwa wameongeza kozi ya Tehama lakini pia wanatarajia kuanzisha kozi ya ufundi wa pikipiki ili kuhakikisha wanamgusa kila kijana ili waweze kujitegemea.
Mwanafunzi, Safia Hamis Mwinyi, kutoka Zanzibar, ameishukuru Serikali ya Mapinduzi kwa kuwafadhiri na anaamini elimu hiyo itaenda kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuwaondoa kwenye utegemezi na kuweza kuwasaidia wazazi wao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...