Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla akizungumza wakati wa kufunga jukwaa la nne la Afya kidigitali na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila Novemba 16, 2024 jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla akizungumza wakati wa kufunga jukwaa la nne la Afya kidigitali na Ubunifu lililofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila Novemba 16, 2024 jijini Dar es Salaam
Mwananfuzi kutoka shule ya Sekondari ya Amos Makala, Isack Mpore akizingumza katika jukwaa hilo.

SERIKALI kupitia wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,imesema itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo ili kuimalisha mfumo wa Afya kidigitali kupitia makubaliano yaliyofanyika kati ya sekta binafsi na umma ilikuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.

Hayo yameelezwa Leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla wakati akifunga jukwaa la nne la Afya kidigitali na ubunifu nchini, lililofanyika katika chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) na kushirikisha wanafunzi kutoka vyuoni na shule mbali mbali za sekondaru.

"Kama mnavyojua mheshimiwa Rais Samia alizindua mpango mkakati wa miaka 10 moja kati ya mikakati ni kuwa na jamii ya kidigitali kwahiyo watu wa MUHAS wameanza kutekeleza adhima hiyo kwa kupitia jamii namba ambayo serikali imeamua itolewe mtoto anapozaliwa na hadi sasa zaidi ya wananchi milioni 20 wanayo,"amesema Abdulla

Ameongeza,"muda umefika wa sekta ya afya kutumia mfumo huo ilikuweza kupata kumbukumbu zote za mtu anaeumwa katika hospitali yeyote nchini ili mgonjwa anapofanyiwa vipimo Muhimbili anapokwenda hospitali nyingine asiwezekufanya vipimo upya,"amesema

Naye,Deodatus Kakoko Mkuu wa shuke ya Afya ya jamii Muhas amesema ni muhimu sana kwa sekta ya afya kuamia kwenye mfumo huo kwani kunaongeza ufanisi katika kazi.

"Mwanzo tulinza na idadi ya watu 10 lakini kadri miaka inavyokwenda watu wanazidi kuongezeka upande wa bara hadi kufikia zaidi ya 400 huku visiwani wakiwa 300 natuma amini wigo utaendelea kupanuka zaidi kwani afya ni ndiyo nguzo mhimu,"amesema...

Kwa upandewake mwanafunzi Isack Mpore kutoka shule ya Sekondari ya Amos Makala amesema katika jukwaa hilo amejifunza kuwa kwa sasa teknolojia ipo mikononi mwa mtu na si kutembea umbali mrefu kama ilivyokuwa hapo awali kwani mtu anapohitaji kujua afya yake huweza kutumia kuzungumza na daktari kisha msaada wa kile anachohitaji kwa muda sahihi.

Pia amewaasa wanafunzi wanapopewa simu watumie kwa mahitaji sahihi kama kujua afya zao na si vingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...