Waziri wa Habari,Mawasiliano  na Teknolojia ya Habari Jerry Slaa akizungumza na waandishi habari kuhusiana  na wahalilfu wa mitaondao,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambi ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa Habari  kuhusiana  na mikakati ya kikosi kazi kitakachundwa katika udhibiti wa wahalifu wa mitandao,jijini Dar es Salaam.
Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma wa simu za mikononi pamoja watumishi wa serikali katika taasisi mbalimbali mara baada ya kufungwa kwa majadiliano ya uhalifu katika mitandao,jijini Dar es Salaam.

*Na wale wa uhalifu kwa njia ya internet ya kudhalilisha utu wa watu
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SERIKALI imesema kuwa kutokana na uhalifu katika mitandao inaunda kikosi kazi kwa ajili ya wahalifu hao wakiwemo matapeli wa kwa njia ya simu mikononi.

Kikosi hicho kitakuwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Maendeleo ,jinsia ,Walemavu na Makundi Maalum Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria ndio zimeunda kikosi kazi kitakacholeta suluhu ya uhalifu wa mtandaoni.

Kikosi kazi hicho kitaanza kazi mara moja kwa kushirikiana na makatibu wakuu wa wizara hizo, wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wizara ya Katiba na Sheria na zingine.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni katika kikao cha mashauriano na wadau kuhusu uhalifu wa mtandao nchini.

Alisema kikozi kazi kitashirikiana na wajumbe kutoka serikalini na wadau wengine kushughulikia changamoto hiyo inayosababisha wananchi wengi kutapeliwa.

"Tunaamini kwa utaratibu huo tutafanikiwa kupambana na changamoto hiyo kwa haraka zaidi hususani kwa mikoa inayoongoza kwa uhalifu mtandaoni ambayo ni Mbeya, Dar es Salaam, Rukwa na Morogoro," alisema.

Masauni alisema kuna haja ya kushirikiana kwa sababu vita ya uhalifu mtandaoni inakua kwa kasi na mbinu zake zinaimarika kwa kasi, hivyo lazima waunganishe nguvu kukabiliana nayo.

Alisema serikali kukabiliana na changamoto hiyo imejipanga kufanya uwekezaji wa rasilimali watu na vitendea kazi , tija ipatikane.

Kwa upande wake , Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa alitoa maagizo manne kwa wananchi kukabiliana na changamoto hiyo.

Wizara hiyo iliwataka wananchi kuhakiki namba zao za nida zilizosajiliwa katika mitandao yao ya simu na kupokea maelekezo kutoka kwa mamba 100 pekee kutoka kampuni za simu.

Pia aliwataka inapotokea tukio la uhalifu mtandaoni kutoa taarifa kituo cha polisi kwa hatua za kijinai.

Pia aliwashauri wananchi kutotoa nywila au mamba zao za siri kwa watu wengine kuepusha utapeli.

Silaa alisema wizara yake itaendelea kusimamia sera ya Tehama na ikibidi kufanyiwa marekebisho watafanya ili kuakisi mwenendo wa sekta ya mawasiliano ambayo inakua kwa kasi.

Hatahivyo alisema kwa kushirikiana na wadau watafanikiwa kuondoa kadhia hiyo mtandaoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...