WANANCHI waaswa kutowakimbia wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakidhani kuwa wanaenda kufunga biashara zao.

Wamewataka wateja wao kutoa maoni yao na kupata elimu kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari.

Hayo yamesemwa na Meneja Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Paul John Walalaze alisema wanahudumia wateja wao mlango kwa mlango kwa kuwaelimisha walipakodi.

Amesema wanakusanya maoni na kuelimisha kuhusu ulipaji kodi na kufanya makadirio ya kodi kwa wateja wao.

"Tunataka wawapatie mashine za kielektroniki za EFD kutoa risiti, kuna umuhimu kulipa kodi, dawa hospitalini, mikopo elimu ya juu, elimu bure,"

Amesema wananchi wakilipa kodi wataweza kuleta maendeleo nchini.

Elizabeth Lakuya Furniture alisema kuwa kila mfanyabiashara anapaswa kuzingatia maelekezo kwa kutoa risiti kwa wateja wao ili kutopata usumbufu.

Alisema inawasaidia kutoa kitu halali na mteja kibali halali kutokana na bidhaa aliyonunua.

Jimmy Ngaiza kutoka Fast Food and Bites amesema wafanyabiashara wanapaswa kuwa tayari kuwapokea TRA

Amesema hali imebadilika walikuwa wakifunga biashara zao pale wanapoona maofisa wa TRA.

Ameeleza maboresho ya kodi yanawasaidia katika kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...