Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt Thomas Bwana Akizungumza na wadau wa Mbegu katika Warsha iliyofanyika Dodoma.
Mkurugenzi idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Bw. Nyasebwa Chimagu Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha iliyofanyika Dodoma
Picha za baadhi ya washiriki  katika warsha.

Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika warsha .
Mkurugenzi idara ya Uhaulishaji wa Teknolojia na Mahusiano Dkt. Sophia Kashenge akitoa wa wasilisho katika warsha

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Thomas Bwana amezieleza kampuni za mbegu kulipia mirabaha ya mbegu wanazotumia zinazotokana na kazi za watafiti wa TARI ili kutoa motisha kwa wagunduzi wa mbegu bora wanazouza kwa wakulima.


Dkt. Bwana amesema hayo leo Novemba 19, 2024 katika ufunguzi wa warsha ya siku moja ya mfumo wa kidigitali wa upatikanaji mbegu na usajili wa mbegu iliyofanyika Dodoma.


Warsha hiyo imewakutanisha Kampuni za Mbegu, wazalishaji wa mbegu, Taasisi mbalimbali za Kilimo na Watafiti ikiratibiwa na TARI ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa AVISA unaolenga kuchochea matumizi ya mbegu bora zilizogunduliwa.


Akieleza kuhusu shughuli zinazofanywa na TARI Dkt. Bwana amesema TARI inafanya utafiti na kutoa matokeo ya utafiti kwa wadau wa kilimo pamoja na kushauri watunga sera kuhusu masuala ya Kilimo lengo ikiwa ni kuongeza tija. ‘’ Watafiti wanafanya kazi kubwa ya ugunduzi wa Mbegu bora za Mazao mbalimbali ambazo nyie kampuni kama wadau muhimu wa Kilimo mnaziuza kwa Wakulima hivyo sio vibaya mkitoa motisha kidogo kwa Watafiti"


Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha hiyo, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Bw. Nyasebwa Chimagu amesema ugunduzi wa mbegu bora unachangia tija katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo ikiwemo utoshelezaji wa chakula, usalama wa chakula na hivyo kufikia ajenda ya Kilimo Biashara ya 10/30.


Bw. John Julius- Mkurugenzi Kampuni ya Mbegu ya TEMNAR iliyopo Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara amesema suala la kulipia mirahaba ni jambo muhimu na linafahamika huku akishauri kujipanga pande zote TARI na kampuni watumiaji kujadili namna njema ya ulipaji mirabaha


Bw. Julius ameeleza kunufaika na warsha hiyo kwa kujifunza fursa pana zilizopo katika sekta ya Mbegu.


Mradi wa AVISA ulianza mwaka 2019 ukitekelezwa na TARI kwa kushirikiana na Taasisi zingine kama Shirika la Kimataifa la Uboreshaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT), Kituo cha kimataifa cha Utafiti wa Kilimo katika nchi za Kitropiki (CIAT), Kituo cha Syngenta na kituo cha Mawasiliano na Ubadilishaji wa Tabia (CBCC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...