Na Mwandishi wetu
Wananchi wa Mtwara wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha zilizopelekea maboresho makubwa ya Bandari ya Mtwara.
Rais Samia ametoa fedha zilizopelekea Bandari kupanuliwa na ununuzi wa mitambo.
"Leo hii tunaona meli kubwa kubwa zikiingia Bandari ya Mtwara, tunaona mitambo mikubwa ya upakiaji na ushushaji wa mizigo ni kazi kubwa ya Rais Samia aliyotufanyia Wana Mtwara." Alisema Said mkazi wa Bandari.
"Sisi wana Mtwara tunajivunia Rais Samia kwani ametukomboa Wana Mtwara asitokee Mtu akajitapa eti amefanya yeye ama bila ya yeye Bandari isingeboreshwa. Amefanya kwa fedha zake? Yeye ndio ameidhinisha fedha za utekelezaji? Iweje ajitape? Sisi wana Mtwara tunajua kazi ya maboresho ya Bandari fedha imeidhinishwa na Rais Samia na yeye ndio anaetoa maelekezo ya utekelezaji wa maboresho ". Alisema Hajra mkazi wa Chikongola.
Rais Samia hivi karibuni alitoa kauli Korosho isafirishwe Bandarini na akahakikisha anapeleka vifaa vipya vikiwemo kreni mbili za rununu, mashine kushughulikia makasha matupu "reach stackers" na Tag Boats za kisasa. Wana Mtwara wanasema Ahsante sana Rais Samia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...