Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema wanachama wa Chama hicho wakishapiga kura warudi nyumbani kusubiria matokeo kwakuwa kuna mawakala wa kulinda kura zao na wanawaamini.

CPA Makalla ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi na wanaCCM wa Jimbo la Kinondoni ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika Novemba 27,2024.

Akiwa katika Jimbo la Kinondoni ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi na hasa wanaCCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kushinda kwa kishindo na baada ya kupiga kura warudi nyumbani kwakuwa mawakala wao watalinda kura hizo.

"CCM tunao mawakala wetu ambao watakuwa katika vituo vya kupiga kura tunawaamini na ndio watakaolinda kura.Hivyo mwanaCCM ukishapiga kura rudi nyumbani.Tumewasikia wenzetu wakiwaambia watu wao walinde kura zao, hawaamini makawala wao."

CPA Makalla amesema katika Mkoa wa Dar wa Salaam amefanya kampeni katika Jimbo la Temeke, Kigamboni, Segerea, Kawe,Ukonga, Ubungo na Kinondoni wakati jimbo la Mbagala Katibu Mkuu wa CCM Dk.Emmanuel Nchimbi ndio atahitimisha kampeni na viongozi wengine watakuwa mikoani.

Hata hivyo amesema kwa kampeni ambazo zimefanywa na Chama hicho tangu Novemba 20 walipozindua kampeni maelfu ya wapinzani wamejiunga na Chama hicho huku baadhi ya wagombi ya wagombea wa upinzani nao wakiomba kuja CCM.

CPA Makalla ametumia mikutano yake ya Kampeni kueleza wananchi kwa kazi ambayo Serikali ya CCM imefanya katika kuleta kuleta maendeleo ya Watanzania imefanya Chama hicho kujihakikishia ushindi wa kishindo kwani kinabwebwa na mazuri yaliyofanyika kupitia urejelezaji wa Ilani.

"CCM haihitaji kubebwa kwani inabebwa na kuuzwa na kazi nzuri zinavyofanywa na madiwani Wabunge na Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema na kusisitiza katika uchaguzi huo wagombea wa Chama hicho wako tayari kuwatumikia Watanzania.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...