Na Mwandishi Wetu Michuzi TV
KAIMU Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala, Tabu Shaibu, amewashauri wanawake wote kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili ziwasaidie kujiinua kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi
Ushauri huo umetolewa leo Novemba 1,2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bajaji inayotumia nishati ya umeme wa jua( Solar) kwa wanawake wanufaika wa mradi wa 'She drive to change' waliopatiwa mafunzo ya udereva kwa ufadhili kutoka Ujerumani
" Niwapongeze sana shirika la Ladies Joint Forum( NGO), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Ujerumani kuweza kuwafundisha wanawake 30 udereva na wote na kuwapatia leseni huku mkiangalia namna ya kuwapatia vyombo vya usafiri ili waweze kujiinua kiuchumi mimi naamini mwanamke ndiye mwangalizi wa familia akiwezeshwa anaweza kuinua na wengine" amesema Tabu
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ladie Joint Forum Francisca Mboya amesema bajaji hiyo iliyozinduliwa wanufaika wa mradi wa She dreve to change ambapo watajipatia kipato na wataendelea kuongeza bajaji nyingine kupitia fedha mbalimbali watakazochangiwa na wadau.
" She drive to change ni mradi wa miezi 12 uliolenga kuwezesha na kukuza.uhuru wa kiuchumi wa wanawake 30 wenye umri wa miaka 18-40 katika kata ya Vingunguti Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam na unazingatia hasa wahanga walionyanyaswa kijinsia,kina mama vijana walemavu na wale wanaolea watoto wenye ulemavu peke yao" amesema Francisca
Kwa upande wake Mnufaika wa mradi huo Oliva Mushi amesema yeye amemudu familia kwa kulipia ada ya shule watoto wake , anajitegemea kwani hapo awali alikuwa anaishi wa ndugu ila tangu amepatiwa leseni anaendesha bajaji na amewashauri wanawame wengine wasikate tamaa ya mafanikio kwani hayapatikani kwa siku moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...