Waziri Mambo ya Nje na Uashirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa Tanzania ikiwa ni mwasisi wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Mkuu (ICGLR) itaendelea kushirikiana na nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo na Jumuiya ya Kimataifa katika juhudi za kutafuta amani ya kudumu kwenye ukanda huo.

Waziri Kombo ameeleza hayo alipozungumza katika Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.

Akizungumzia kuhusu msimamamo, mchango na nafasi ya Tanzania katika kufatua amani na usalama kwenye ukanda wa Maziwa Makuu Waziri Kombo ameeleza kuwa, Tanzania chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itafanya kazi bila kuchoka kwa kushirikiana na nchi wanachama na Jumuiya ya Kimataifa kutatua migogoro iliyopo ili kuwa na ukanda wenye amani, ustawi na ustahimilivu.

“Kama mwanachama mwanzilishi wa ICGLR, Tanzania inaamini kuwa kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia na kuimarishwa kwa utulivu kutaongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi ya watu wetu katika Ukanda wa Maziwa Makuu” Ameeleza Waziri Kombo.

Aidha, Waziri Kombo licha ya kueleza utayari wa Tanzania katika kuendelea kushirikiana na wadau katika kurejesha amani na usalama kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, ametoa wito kwa nchi wanachama kuhakikisha kuwa ushawishi wa washirika wa maendeleo hauathiri utendaji na ufanisi wa mifumo iliyowekwa ikiwemo Mfumo wa Tahadhari ya Mapema na Majibu ya Migogoro wa ICGLR (ICGLR Conflict Early Warning and Response Systems).

Vilevile, amesisitiza umuhimu wa nchi Wanachama kuheshimu na kutimiza wajibu wake wa kuchangia fedha kwa Sekretarieti, ikiwa ni ishara ya mshikamano na juhudi za pamoja, katika kuhakisha Jumuiya inatekeleza mipango na mikakati inayojiwekea ili kufikia matarajio ya kuwa na ukuanda wenye Usalama, Utulivu, na Maendeleo endelevu.

Pia ametumia fursa hiyo kuitaka Sekretareti ya ICGLR kuzingatia matumizi mazuri na usimamizi mzuri wa fedha kwa manufaa ya kanda.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Balozi Téte António akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ameleeza ameeleza kuridhishwa kwake na mazungumzo yanayo endelea yakilenga kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na DRC.

Aliendelea kutoa wito kwa nchi wanachama kwa umoja wao kuendelea kushughulikia changamoto zinazotishia amani, usalama, na hali ya kibinadamu katika Jamhuri ya Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, na ghasia zinazoendelea katika Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote 12 Wanachama wa Maziwa Makuu na Mjumbe Maalumu kutoka Umoja wa Mataifa anayesimamia Ukanda wa Maziwa Mkuu Balozi Huang Xia.

Waziri Mambo ya Nje na Uashirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024. 

 

Balozi wa Tanzania nchini Angola mwenye makazi yake nchini Zambia Mhe. Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule akifuatilia Mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliokuwa ukiendelea jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Mhe. Musalia Mudavadi Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya (Prime Cabinet Secretary) wafurahia jambo pembezoni mwa mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Mhe. Balozi Téte António kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kawaida wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi Wanachama wa ICGLR uliofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 24 Novemba 2024.
Mkutano ukiendelea
Picha ya pamoja
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...