Wizara ya Nishati imetumia jukwaa la Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika unaofanyika Jijini Cape Town Afrika ya Kusini kueleza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya nishati Tanzania na kukaribisha wawekezaji kuchangamkia fursa hizo.
Wizara kupitia wasilisho lililofanywa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio Novemba 05, 2024 ilibainisha fursa katika maeneo mbalimbali yakiwemo uwekezaji katika vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia, miundombinu ya mafuta na gesi, miradi ya nishati jadidifu na viwanda vya petrokemikali.
Kwa upande wa vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia, Dkt. Mataragio alieleza kuwa tayari Wizara imekamilisha maandalizi muhimu kuelekea tukio la uzinduzi wa duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia vilivyo wazi, tukio ambalo litazinduliwa rasmi Machi, 2025 wakati wa Mkutano na Maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jijini Dar es Salaam.
“Tunatarajia kunadi jumla ya vitalu 26 vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Kati ya vitalu hivyo, vitalu 23 vipo eneo la baharini na vitatu (3) vipo eneo la ziwa Tanganyika” alieleza Mataragio.
Pamoja na vitalu hivyo, Mataragio alieleza kuwa ipo fursa kwa wawekezaji kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuendeleza vitalu vya Eyasi-Wembere, Mnazi Bay Kaskazini na Songo Songo Magharibi; vitalu ambavyo TPDC imeendelea kuvifanyia utafiti wa mafuta na gesi asilia.
Katika wasilisho, Mataragio alieleza kuwa data za vitalu vyote (vitakavyopelekwa katika mnada na vile vinavyoendeshwa na TPDC) zinapatikana kwa wawekezi kuona na kununua. Miongoni mwa aina za data alizozitaja ni pamoja na data za nguvu sumaku ya miamba (magnetic), uzito wa miamba (gravity), mitetemo (2D na 3D) na visima.
Maeneo mengine ya uwekezaji aliyoyataja katika sekta ndogo ya mfatuta na gesi asilia ni uwekezaji katika ujenzi wa vituo vya kujaza gesi asilia kwenye magari na viwanda vya petrokemikali kwa kutumia gesi asilia.
Pamoja na kueleza fursa zilizopo, Dkt. Matarajio alieleza kuwa Serikali imefanya kazi kubwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kutekeleza miradi ya kimkakati kama vile Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), hivyo Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio akifanya wasilisho kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati Tanzania wakati wa Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika unaofanyika Cape Town Afrika ya Kusini.

Kamishna wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati Bw. Goodluck Shirima (watatu kushoto), Kamishna Msaidizi wa Petroli Wizara ya Nishati Mha. Joyce Kisamo (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mha. Charles Sangweni na washiriki wengine waliohudhuria wakifuatilia wasilisho la fursa za uwekezaji nchini Tanzania. Wasilisho hilo lilifanywa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio wakati wa Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika unaofanyika Cape Town Afrika ya Kusini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Mussa Makame (mwenye miwani na baadhi ya viongozi kutoka TPDC wakifuatilia wasilisho la fursa za uwekezaji nchini Tanzania. Wasilisho hilo lilifanywa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio wakati wa Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika unaofanyika Cape Town Afrika ya Kusini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya mafuta na gesi, Dkt. James Mataragio akifanya wasilisho kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati Tanzania wakati wa Mkutano wa Wiki ya Nishati Afrika unaofanyika Cape Town Afrika ya Kusini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...