Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mwajabu Nyamkomora (kulia) akikata utepe kuzindua rasmi duka jipya la Airtel ndani ya kituo cha SGR mjini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adrianna Lyamba. Duka la Airtel SGR Station mjini Dodoma linatoa huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa laini za simu, huduma za fedha za Airtel Money, mauzo ya simu kwa njia ya mkopo na kutoa huduma zote za mawasiliano kwa wateja.
.jpeg)
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mwajabu Nyamkomora (wa pili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adrianna Lyamba (wa kwanza kulia) wakati wahafla maalum ya kuzindua duka jipya la Airtel Tanzania ndani ya kituo cha SGR mjini Dodoma. Kufuatia uzinduzi huo, Airtel sasa inafikisha jumla ya maduka 45 nchi nzima ikiwa ni jitihada za kampuni kufikisha huduma kwa wateja kote nchini.
AIRTEL Tanzania imezindua duka la tatu la SGR mjini Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa kutimiza dhamira ya Airtel ya utoaji wa huduma bora kila mahali nchini. Duka jipya la Airtel SGR Station litatoa huduma zote za Airtel kwa wasafiri, wafanyabiashara wanaopita katika kituo hicho cha SGR Dodoma pamoja na wakazi wa eneo hilo, Airtel tayari ilishazindua pia maduka mengine ya Airtel kwenye vituo vikuu vya SGR kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.
Kupitia uzinduzi huu, Airtel Tanzania itakuwa imefikisha jumla ya maduka ya huduma kwa mteja 45 yalivyosambaa nchi nzima ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zote za Airtel katika maeneo ya mijini na vijijini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Msaidizi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Mwajabu Nyamkomora aliipongeza Airtel Tanzania kwa jitihada zake za kuboresha mawasiliano nchini.
“Airtel Tanzania imeendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika ukuaji wa maendeleo ya kidijitali na sekta ya mawasiliano nchini. Duka hili ni ishara ya kuunga mkono maono ya serikali ya kuhakikisha huduma zote muhimu zinawafikia wananchi na kuchagiza maendeleo ya taifa,” alisema Nyamkomora.
Duka la Airtel SGR Station mjini Dodoma linatoa huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa laini za simu, huduma za fedha za Airtel Money, mauzo ya simu kwa njia ya mkopo na kutoa huduma zote za mawasiliano kwa wateja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania Bi, Adrianna Lyamba alisisitiza juu ya nia ya Airtel kuwapa kipaumbele wateja wake.
“Tunajivunia kuwa mtoa huduma ambae anamjali zaidi mteja wake. Mahitaji ya wateja wetu ni kipaumbele chetu, Duka hili ni zaidi ya kituo cha kutolea huduma kwasababu ni alama ya kuimarisha huduma zetu Pamoja na kujenga mahusiano imara na wateja wetu na kuendeleza ubunifu ili kufikia mahitaji yao yanayoendelea kukua kila wakati,” alisema.
Duka la Airtel SGR Station limewekwa kimkakati kwenye kituo cha usafirishaji kwa lengo la kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuboresha miundombinu ya kisasa na kuimarisha hali ya mawasiliano nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...