Na Farida Mangube Morogoro
Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa soko kuu wa Chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro wametakiwa kuhama katika vibanda hivyo kwa madai kuwa vipo katika eneo sio rasmi.
Wakizungumza na Muchuzi Blog Wafanyabiashara Hawa wamesema disemba 5 mwaka huu wamepewa barua za kuhama katika eneo hilo na kutakiwa kuhamia eneo la nyuma ya soko jambo ambalo wao wanaona linawapa changamoto hasa kupata wateja.
Wanasema licha ya eneo hilo kutokuwa rafiki Kwa wateja lakini pia tayari vibanda hivyo waligaiwa watu wengine hivyo hofu Yao kuingia migogoro na wafanyabiashara wengine.
Changamoto hiyo imemlazimu Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdu lazaz Abood amefika ksokoni na kuzungunza na wafanyabiashara ambapo amewataka Kuwa watulivu Kwa muda wakati serikali inashughulikia changamoto hiyo
Mhe. Abood amesema ni lazima Serikali kabla ya kuwaondoa itenge eneo Maalum ambalo litakuwa rafiki kwaoili waweze kufanya biashara kama kawaida bila kuathiri mitaji yao.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan anapenda vijana kujiajiri hivyo yeye kama Mbunge hatukubali suala hilo kwani wengi wao wanekupa fedha za asilimia Kumi NJ lazima wawekewe mazingira rafiki.
Akitolea ufafanuzi suala hilo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaaa ya Morogoro Lilian Heneriko amekiri wafanyabiashara hao kupewa notisi ya kuhama katika eneo hilo Ili kipisha ujenzi wa uzio na miundombinu mingine ya kiusalama.
Amesema eneo hilo linamachinga 500 hivyo wataondolewa ni 94 tuu na watahamishiwa eneo la nyuma ya soko sio watahamishiwa moja Kwa Moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...