💥Ni kutokana na mchango wake Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa wamempatia Tuzo Maalum Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Salim Abri Asas wakitambua mchango wake hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comrade Daud Yassin mara baada ya kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa leo Disemba 21, 2024.

"Amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye chama hapa Mkoani kwetu Iringa, tunamshukuru na kumpongeza sana. Kutoa ni moyo sio utaajiri, kazi yetu ni kumwombea afya njema," amesema Yassin.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa kwa umoja wao wakichangia mada mbalimbali walimpa pongezi MNEC ASAS kwa kujitokeza kwake kuimarisha CCM.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...