Na WMJJWM - Dar Es Salaam.

Serikali ya Tanzania imetia saini ya mkopo wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 104 kutoka Benki ya Dunia ili kutekeleza Mradi unaoitwa PAMOJA wenye lengo la kuwawezesha Wanawake Kiuchumi na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia.

Hafla hiyo ya utiaji saini  imeongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nathan Belete na kushuhudiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima leo Desemba 12, 2024 jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema, Wizara ya Fedha itashirikiana moja kwa moja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii katika kuleta usawa wa kijinsia na kwamba, kusainiwa kwa mradi huo kutasaidia utekelezaji wa Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023) kwa kuwa maeneo ya kipaumbele ya mradi,ambayo ni kuwezesha  wanawake kiuchumi, kuzuia na kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Naye Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Nathan Belege ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza juhudi za kuleta usawa wa kijinsia, hivyo Benki ya Dunia itaendelea kutoa ushirikiano na Tanzania kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa wanawake.

Kwa upande wake, Waziri Dkt. Gwajima  amesema tayari Tanzania imeshazindua Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023) na Mkakati wake ambapo, malengo ya mkopo huo yanatafsiri yaliyomo kwenye Sera hiyo.  

Aidha, amesema mradi huo utatekelezwa kwa pande zote mbili za Tanzania Bara na Zanzibar ambapo, nyumba salama zitajengwa kwa manusura wa ukatili, vituo vya malezi na makuzi ya watoto wa umri wa awali, Ofisi za Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamiii na vitendea kazi kwa Maafisa hao.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...