Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji magari nchini ya Ezy Auto Motors Bi. Upendo Ngogo ameagiza watendaji wa mauzo katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kuendelea kunufaisha wateja wao kupitia punguzo kubwa la bei sambamba na kutoa zawadi mbalimbali.

Amesema hayo Novemba 29, 2024 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wafanyakazi wake wa mauzo wa matawi mbalimbali ya kampuni hiyo ambayo ni Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma na Geita na kuwasisitiza kuongeza juhudi katika kutoa huduma bora kwa wateja.

Bi. Ngogo amesema kuwa, kuanzia mwezi Disemba hadi Januari 2025 kampuni itatoa punguzo kubwa la bei kwa wateja wote wanaonunua magari, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea msimu wa sikukuu na kutoa fursa kwa watu wengi kumiliki magari. Punguzo hilo litaanzia kati ya shilingi 500,000 hadi 1,500,000 kwa kila gari kulingana na aina na thamani ya gari.

Vilevile, Bi. Ngogo amesisitiza kuwa kila mteja atakayenunua gari katika kipindi hicho ataondoka na kapu la zawadi linalojumuisha vitu mbalimbali kama vile triangle, fire extinguisher, kikombe cha safari, mwamvuli, huduma ya bure ya kurekebisha gari, mafuta na bima za magari.

Katika kuhakikisha urahisi wa malipo, mteja anaweza kuanza na kiasi kidogo cha asilimia 30 tu ya gharama ya gari, kisha kulipa kiasi kilichobaki kuingia makubaliano ya mikopo ya hadi miaka miwili ili kutoa fursa kwa wateja kumiliki gari hata kwa gharama za awali huku wakiendelea kulipa kwa urahisi.

Ezy Auto Motors imekuwa miongoni mwa kampuni zinazoongoza katika uuzaji wa magari kutoka nje ya nchi hapa nchini, ikijivunia utoaji wa huduma bora, bei nafuu, na mikopo rafiki kwa wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...