TAARAB Kunogesha Usiku wa Tamasha la Mkesha wa Sikukuu ya Christmas "ONJESHA EXPERIENCE CHRISTMAS EVE" huku Watoa burudani Sabah Muchacho Akili the Brain ndani ya Khana Khazana Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa Kutambulisha Tamasha hilo Mtayarishaji na Msanii wa Muziki wa Bongofleva kwa aina ya Mahadhi ya Kihindi "Akili the Brain" amesema kwa mara ya kwanza Tamasha hilo linakwenda kufanyika Disemba 24,2024 lengo ni kukaribisha Sikukuu ya Christmas 2024 kwa Mashabiki wa Taarab na Bongofleva kwa pamoja.

Aidha Ameongeza kuwa Usiku huo utakuwa wa kipekee kwani Mashabiki watashuhudia na kusikiliza Miziki hiyo miwili inavyoingiliana na kuupamba usiku huo huku Mashabiki watarajia kolabo kutoka kwake na nguli wa Muziki wa Taarab Sabah Muchacho pamoja na Ep yao.

Kwa Upande wake Sabah Muchacho amewaomba Mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hilo huku akitolea ufafanuzi swala la baadhi ya Mashabiki wa nyimbo zake kutumia kama sehemu ya kufanya ugomvi katika kumbi za starehe.

''Kwa sasa Kumekuwa na Wimbi Kubwa la baadhi ya wapenzi wataarab kutumia nyimbo zetu kugombana au kurushiana ngumi sio kitendo kizuri kwani hizi tungo tumezitunga kwa ajili ya kurushana roho lakini sio kutoana roho."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...