Na Mwandishi wetu, Mirerani
MAELFU ya wakazi wa mikoa ya Manyara na Arusha, wamejitokeza kwa wingi kumzika mwana mazingira maarufu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, Amos Simon Saitore Kaaya ambaye alifariki dunia hivi karibuni.
Angelflower Kaaya ambaye ni mmoja kati ya watoto wa marehemu Amos Kaaya, akisoma historia ya marehemu baba yao amesema alizaliwa Novemba 11 mwaka 1955 kwenye kijiji cha Mikungani wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Amesema baba yao alikuwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 14 wa mzee Simon Kaaya, ambapo alibatizwa mwaka 1956 na kupata kipaimara mwaka 1969 katika usharika wa Mbuguni mtaa wa Mikungani.
“Mzee Amos alifunga ndoa takatifu ya Kikristo na mke wake Veronica Sifael katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mirerani Cairo na baba amebarikiwa kupata watoto saba na mmoja ni marehemu na kwa baraka nyingi za Mungu uzao wake amebarikiwa kupata wajukuu 16,” amesema.
Amesema mwaka 1963 alipata elimu ya msingi shule ya Mikungani na elimu ya kati Makumira middle school kisha akajiunga na chuo cha uchapishaji Same mkoani Kilimanjaro.
“Alikuwa Baba bora, alipenda kujiita Kaaya na watoto, mlezi na mshauri wa kila mtu, watu wengi hata hapa tulipo wamepitia katika mikono ya mzee huyu bila kujali kabila, umri wala dini yake,” ameeleza.
Amesema baba yao alikuwa mpenda maendeleo alishiriki katika maendeleo ya familia yake na jamii kwa ujumla tangu mwaka 1978 hadi 1982 alikuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) Mirerani.
“Alikuwa mtu wa watu kila mmoja hapa ataweza kuhadithia ucheshi wa mzee, utani wake, ukarimu wake kwa kila mtu hata kupeana majina y autani kaka Paflaz, kalan Ndauo, Kaaya na watoto, bwana mazingira, habari zenuuu, jamaa yangu na mingine mingi hata wauza mbogamboga wa Mkuyuni walimwita mbunge wao," ameeleza.
Stella Amos Kaaya ambaye ni mtoto mkubwa wa marehemu Amos Kaaya amewashukuru wauguzi na madaktari wa kituo cha afya Mirerani, hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma na hospitali ya KCMC kwa jitihada walizozionyesha kuokoa uhai wa baba yao.
“Idadi ya watu mnayoiona leo, wote wameletwa kwa upendo wa mzee Amos na tunaomba kila mmoja achukue dakika moja kumwombea pumziko la milele, huu siyo msiba wa mzee Amos ila ni sherehe ya mzee Amos,” amesema.
Mkuu wa jimbo la kusini mstaafu, Dayosisi ya Meru, Zelothe Palangyo akizungumza kwenye mazishi hayo amemwelezea marehemu Amos Kaaya kuwa alikumbusha jamii kuheshimu uchaji wa ibada kwa kuzima simu wakati wa ibada.
Mchungaji Palangyo amesema marehemu Amos Kaaya hata akiwa kitandani kipindi cha ugonjwa wake aliendelea kutuma sadaka zake kanisani kwa uaminifu.
Mchungaji kiongozi wa usharika wa Mikungaji mtaa wa Mirerani Cairo, Humphrey Kisanga amesema marehemu alikuwa mcha Mungu aliyejitoa kwa hali na mali katika kumtumikia Mungu.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amemwelezea marehemu Amos Kaaya kama mtu mpambanaji aliyejitoa kuwasomesha watoto wake kwa kiwango cha kuwa na shahada moja hadi mbili.
“Marehemu Amos Kaaya nimemfahamu kwa miaka mingi ambapo familia zetu zilikuwa marafiki na kama ndugu ambao tuliishi kwa amani na upendo,” amesema Ole Sendeka.
Mwenyekiti wa mtaa wa Cairo, Gadi Msuya amesema marehemu Amos Kaaya atakumbukwa kwa kushirikiana na jamii kujitoa katika maendeleo mbalimbali ya eneo hilo.
Mchungaji Lazaro Urio akizungumza wakati wa kuvunja matanga amewataka watoto wa marehemu kupendana na kuendeleza umoja aliowaachia baba yao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...