Na Jane Edward,Arusha


Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro(NCAA)imezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi wa makundi mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii vilivyo katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka 2024.Kampeni hii imezinduliwa leo yenye kauli isemayo Mery And Wild Ngorongoro Awaits ambapo inatarajia kuanza mapema leo hadi tarehe 4 January 2025 kwa kushirikiana na kampuni ya Smile Safaris iliyopo katika jiji la Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Mariam Kobelo Meneja wa Idara ya Utalii na Masoko NCAA amesema mamlaka ya Ngorongoro imeamua kuanzisha kampeni hiyo kwa mwaka huu kuweza kuongeza idadi ya watalii wa ndani na kuwezesha watanzania kuwa sehemu ya kufahamu vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Amesema kuwa idadi ya watalii wa ndani wanaotembelea eneo la hifadhi hiyo ni ndogo kulinganisha na wageni wanaokuja kutoka Mataifa mbalimbali duniani hali iliyopelekea kuona umuhimu wa kuwezesha watanzania kutembelea maeneo hayo yanayosimamiwa na hifadhi hiyo.

"Takwimu hii inaonyesha wazi kuwa mwamko wa watanzania kutembelea maeneo ya hifadhi bado ndogo na hivyo kuhitajika  msukumo wa sisi kama mamlaka kufanya jitihada za makusudi za uhamasishaji wa wananchi"Alisema

Akizitaja fursa za watanzania watakazozipata wakati wakiwa katika eneo la hifadhi hiyo ni pamoja na kutembelea kreta ya Ngorongoro,Kreta ya Empakai na Olmoti,Msitu wa nyanda za juu kaskazini ambao ni makazi ya wanyama wengi ikiwemo ikiwemo Simba,Tembo,Faru,Nyati na Chui.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...