SHIRIKA la vijana la Tanzania Youth Vision Association (TYVA) linaungana na taasisi na mashirika mbalimbali yanayoangazia haki na ustawi wa jamii ya watanzania hasa kundi la vijana, kulaani vikali mfululizo na mwenendo wa matukio ya utekaji ama ukamataji usiofata sheria na taratibu za ukamataji nchini.

TYVA imeshuhudia matukio mfululizo ya vijana kutekwa, kuumizwa na kukamatwa kiholela kunakopelekea hofu na taharuki kwa jamii toka Januari hadi sasa, pamoja matukio ya hivi karibuni ya vijana kutekwa au kukamatwa kiholela. Hivyo tukiwa tunaenda kuhitimisha mwaka tunaungana na taasisi za haki za binadamu, wanaharakati wa demokrasia na watanzania wenye mapenzi mema kukemea na kulaani vikali matukio haya mabaya ambayo hayaendani na mila wala tamaduni zetu.

Tanzania Youth Vision Association (TYVA) kama ilivyo dira yetu “Kuona jamii huru, yenye haki, ya kidemokrasia na amani yenye ushiriki na ushirikishwaji wenye tija kwa vijana” ”inalaani vikali matukio hayo yanayotokea nchini;

1. TUNALAANI; Matukio ya utekaji ama ukamataji usiofata sheria na taratibu za ukamataji yanayozidi kushamiri nchini hasa kwa kundi la vijana wanaopaza sauti juu ya utawala bora na usawa wa kidemokrasia nchini. Ikumbukwe bado watanzania hatujapata majibu ya kupotea kwa vijana wengine ambao walikamatwa na watu waliodhaniwa ni Jeshi la Polisi na hawakupatikana mpaka wakati huu.

2. TUNALAANI; Matukio ya utekaji ama ukamataji usiofata sheria na taratibu za ukamataji yanayozidi kushamiri nchini tukiamini yana lengo na nia ovu ya kujaza watanania na vijana hofu kwenye kusimania utawala bora, usawa wa kidemokrasia na uhuru wa kushiriki katika michakato ya kisiasa.

RAI YETU
1. Tunamshauri Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda tume huru itakayo fatilia kwa kina matukio haya mabaya nchini na wahusika wachukuliwe hatua.

2. Tunatoa rai kwa vyombo vyetu imara vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi Tanzania kutolea ufafanuzi wa kina juu wa usalama wa vijana wanaoshiriki siasa nchini, makundi ya watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati ambao wamekuwa

wahanga wakuu wa utekaji ama ukamataji usiofata sheria na taratibu za ukamataji nchini. Hii itasaidia kupunguza umbwe la hofu isiyo na msingi na kuimarisha ushiriki wa vijana kwenye ajenda za kimaendeleo, kijamii na kisiasa nchini.

Pia, tunahamashisha vijana kuendelea kufurahia uhuru wao wa kutoa mawazo na kujumuika kwenye michakato mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii bila woga na kuendelea kujihusisha kikamilifu kwenye matukio muhimu ya kuimarisha kidemokrasia nchini.

Imetolewa na bodi ya wakurugenzi ya TYVA, 

PETER ELIAS MASOI

MWENYEKITI WA BODI YA TANZANIA YOUTH VISION ASSOCIATION

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...