Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Miradi wa TASAF John Steven amewapongeza watu wenye ulemavu kutoka katika Kaya za Walengwa kwa jitihada wanazoonesha katika kupambana na umaskini.

Hayo ameyasema Desemba 3,2024 alipotembelea banda la TASAF la Walengwa wenye Ulemavu katika kuadhimisha Siku ya Watu Wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

"TASAF inafarijika sana kuona mko vizuri katika kupambana na Umaskini na hakika mnautendea haki msaada mnaopewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF", alisema Bw. Steven.

Kwa upande wake Bi. Amina Ally, mkazi wa Mlandizi mwenye Ulemavu wa Miguu, ameishukuru sana TASAF na Serikali kwa kuwashika mkono watu wenye Ulemavu maana ameweza kuanzisha biashara ya kùuza batiki, viungo vya chakula, shanga na karanga.

"Nikikumbuka TASAF ilikonitoa, namshukuru Mungu maana sijui ningekuwa wapi nikifanya nikifanya nini?"

TASAF imeshiriki kwenye maadhimisho hayo kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwake baada ya kuongeza afua ya watu wenye Ulemavu katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Katika maadhimisho hayo, Walengwa wameweza kuonesha mtaalam wao wa kusuka, kufuma, kuchakata viungo vya chakula na utengenezaji wa sabuni za maji kwa mtumizi mbalimbali pamoja na batiki.

Aidha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe Ridhiwani Kikwete na Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Bi Zuhura Yunus ni miongoni mwa waliotembelea Banda la walengwa hao wa TASAF.

Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko akikagua Mabanda katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF akiongea na mlengwa katika banda la TASAF katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani.
Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Bi Zuhura Yunus alipotembelea banda la TASAF katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa diamond jubilee Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe Ridhiwani Kikwete alipotembelea banda la TASAF katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa diamond jubilee Jijini Dar es Salaam leo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...