Kaimu Naibu Kamishna wa walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo akimkabidhi zawadi za shukrani Meneja wa Fedha kutoka kampuni ya uuzaji wa magari ya Jiefang Motors, EllaZheng, wakati Mamlaka ya Mapato walipowatembelea mahali pa kazi jijini Dar es Salaam leo Desemba 19, 2024, kwaajili ya kuwashukuru kuwa walipakodi wazuri.


Kulia ni Meneja Mkuu wa SAS Logistic LTD, Adam Ambar akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya mapato Tanzania wakiongozwa na Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo leo Desemba 19, 2024 walipowatembelea kwaajili ya kuwashukuru kwa kuwa walipakodi wazuri.

Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo akimkabidhi zawadi za shukrani Meneja wa Fedha kutoka kampuni usafirishaji ya SAS logistics, Adam Ambar wakati Mamlaka ya Mapato walipowatembelea mahali pakazi jijini Dar es Salaam leo Desemba 19, 2024, kwaajili ya kuwashukuru kuwa walipakodi wazuri.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania kupitia Idara ya Walipakodi wa Kati leo wamewatembelea na kuwashukuru kampuni ya Usafirshaji wa Mizigo ya SAS Logistic Ltd  iliyopo Tabata Reli, Wasco Isoaf tz ltd Masaki pamoja na kampuni ya uuzaji wa magari  Jiefang Motors Tanzania ilipo Tazara.

Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo akizungumza leo Desemba 19, 2024 wakati wa ziara hiyo amewashukuru walipa kodi hao kwakuwa walipakodi wazuri katika kipindi kilichopita. 

Pia  amewaomba kuwa na ushirikiano na Mamlaka hiyo katika kipindi kipya Cha miezi sita kinachokuja.

"Tunaamini mchango wao ni muhimu kwetu wote na ni muhimu kwa Taifa na ni muhimu kwa Watanzania wote kwa ujumla." Amesema Barongo 

 "Tumekuja hapa kwa mteja wetu, tukiwa kwenye mfululizo wa kuwashukuru walipa Kodi  wetu ambao tumekuwa nao kwa kipindi Cha miezi sita wamekua na mchango mkubwa kwetu na wamekuwa na mchango mkubwa kwa taifa hivyo tumeona ni vyema kuja kuwashukuru kwa mchango huo lakini pia kuwatakia heri ya krismasi na mwaka mpya.

Aidha Barongo ametoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kulipa Kodi kwahiari na kwa wakati,  kwa wale ambao wanatakiwa kulipa kodi ya ongezeko la thamani VAT amewaomba kukamilisha kulipa kwani siku ya mwisho ni kesho  tarehe 20, Desemba 2024 hivyo wahakikishe wanakwenda kulipa Kodi zao.

Kwa Upande wa Meneja Mkuu wa SAS Logistic LTD, Adam Ambar amewashukuru TRA kwa kuwatambua katika kama ni walipaji wa wazuri kwani kodi ni kwaajili ya kuchochea Maendelea ya kila mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.

"Sisi kama SAS Logistics tunashukuru kwani mmetukumbuka mmeona, msingekuja bila kuona... Na sisi tunashukuru kwa kututambua na tutaendelea kuiunga mkono serikali ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi tumejiwekea kwamba hakuna kodi itakayopotea tukiwa sisi tupo hapa kwasababu chakwako chukua cha wenzako wape hiyo kwetu ndio kanuni yetu." Amesema Ambar 

Akizungumzia changamoto wanazozipata kama kampuni ya usafirishaji, Ambar  amesema kuwa kunachangoto katika mizani ya Mikumi 'Check Point' ya uelewa wa watumishi

Akizungumza wakati walipotembelewa ofisini kwao wanapouza Magari, Afisa Mwajili wa FAW, Happy Mjema amewashukuru ugeni wa TRA...

 "Tunawashukuru ugeni wa TRA ulioambatana na Naibu Namishna wa TRA nakutupongeza kwa jinsi tunavyoshirikiana nao vizuri na pia kututakia heri ya krismasi na mwaka mpya katika mwaka tunaolekea wa 2025 tunashukuru sana tunawapenda na karibuni tena." Amesema Happy

Kaimu Naibu kamishna walipa kodi wa Kati kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Godwin Barongo akiwaaga wafanyakazi wa SAS Logistics Ltd  mara baada ya kuwatembelea katika ofisi zao zilizopo Tabata wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania walipowatembelea mahali pa kazi jijini Dar es Salaam leo Desemba 19, 2024 kwaajili ya kuwashukuru kuwa walipakodi wazuri.




Matukio Mbalimbali wafanyakazi TRA wakiwatembelea Walipa kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...