Na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara John Mongella amesema ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita hivi karibuni ni kwa sababu chama hicho kimewatumia vijana kwenda kuongea na vijana wenzao namna ambavyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyofanya kwenye jamii nchini.

Amesema hayo  leo Novemba 30, 2024 Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wakati akifungua mafunzo ya 13 ya Uongozi ya mapitio ya juhudi za kuleta mabadiliko ya kisasa katika nyanja za maendeleo yaliyohusisha vijana viongozi kutoka nchi sita za kusini mwa Afrika katika harakati za maendeleo yaliyofadhiliwa na Chama Cha Kikomunisti cha nchini China (CPC).

Mongela amesema kuwa vijana ni kundi lenye nguvu katika jamii na CCM imebaini hilo na  kuwapa jukumu hilo la kwenda kusema yanayofanywa na serikali yao katika jamii.

Mafunzo hayo yamezinduliwa leo yatahitimishwa Desemba 08, 2024.

Mkuu wa Shule  ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Prof Marcellina Chijoriga amewaelezea washiriki  hao 120  ambao wametoka kwenye vyama  rafiki  Kusini mwa Afrika  ambavyo ni ANC (Afrika ya Kusini), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), ZANU- PF (Zambia) CCM wenyeji  pamoja na CPC ambaye ni mfadhili mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...