Mwandishi Wetu

Wadau wa Nishati Safi ya kupikia nchini, wameitaka Serikali kutunga sera ili kuwabana wanaoingiza vifaa visivyo na ubora kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kupikia.

Hayo yamesemwa Jumatano Desemba 4, 2024 katika hoteli ya Coral Beach wakati wa mkutano wa kujadili sera katika sekta nishati ulioandaliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) na kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na Serikali ili kuangalia ni namna gani jamii inaweza kushirikishwa kikamilifu katika mpango huu wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2034 wawe wanatumia nishati safi.

Meneja wa UNCDF , Imanuel Muro amesema kuna kila sababu ya Serikali kutunga sera ya uingizaji wa vifaa kwa ajili ya matumizi ya nishati safi kwa wananchi.

Baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na majiko ya gesi, umeme, mipira ya kusukumia gesi, stovu pamoja na mitungi.

Amesema Serikali ina taasisi zake kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambalo kazi yake ni kudhibiti ubora wa bidhaa mbalimbali zinazoingizwa nchini, hivyo lisimamie kwa umakini uingizwaji huo.

“Ni vema udhibiti huu ukawepo ili kudhibiti wafanyabiashara wasiokuwa wazalendo ambao wanaweza kuweka vifaa feki sokoni na kuathiri watumiaji,” amesema.

Aidha Muro ameenda mbali zaidi akisema kuwa hata ikiwezekana, ili kuongeza uelewa wa nishati safi, Serikali iingize katika mitaala suala hilo ili wanafunzi wafahamu tangu wakiwa shuleni umuhimu wa mpango huo.

Akichangia katika mazungumzo hayo, Andres Mendes, mdau wa Nishati Safi kutoka Kenya amesema kuna haja ya kupeana taarifa mbalimbali kuhusiana na kila hatua ya mpango huo wa nishati safi wa kidunia ili wananchi waweze kuwa na uelewa wa mpango huo.

Amesema ikiwa hakutakuwa na taarifa na maelezo ya kutosha kuhusu umuhimu wa nishati safi, utekelezaji wake utakuwa hafifu.

Naye Katarina Aloyce anayefanya kazi ya utafiti mbalimbali, amesema kuna haja ya kupunguza gharama kwa kila kitu kinachohusiana na matumizi ya Nishati Safi ili kila Mtanzania aweze kumudu gharama.

Akitoa mfano, amesema kuwa kwa kuwa Serikali imepeleka umeme vijijini, na inahamasisha matumizi ya Nishati Safi, sasa hatua hiyo itakuwa na tija kwa kupunguza gharama kwa vifaa wezeshi vya matumizi ya Nishati Safi ikiwemo nishati ya umeme.

Mpango huo wa UNCDF unafanya kazi ya kuhabarisha na kuibua mijadala namna ya kutekeleza mpango wa nishati safi umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), UNCDF, Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) na CoockFund.

Miongoni mwa walioshiriki mkutano huo ni maofisa kutoka Shirika la Umeme nchini (Tanesco), TBS na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( Ewura)
 

Meneja Mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) Emanuel Muro akizunguzma  katika mkutano wa kujadili sera katika sera nishati ulioandaliwa na  na kuwakutanisha wadau mbalimbali  kutoka sekta binafsi na Serikali ili kuangalia ni namna gani jamii inaweza kushirikishwa kikamilifu katika mpango huu wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2034 wawe wanatumia nishati safi.




 

Baadhi ya picha za matukio katika mkutano wa kujadili sera katika sera nishati ulioandaliwa na  na kuwakutanisha wadau mbalimbali  kutoka sekta binafsi na Serikali ili kuangalia ni namna gani jamii inaweza kushirikishwa kikamilifu katika mpango huu wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania ifikapo mwaka 2034 wawe wanatumia nishati safi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...