Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

WATUHUMIWA sita wanaodaiwa kufanya jaribio la kumteka Mfabyabiashara Deogratius Tarimo wamepelekwa gerezani baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana dhidi ya kosa lao hilo.

Washtakiwa baada ya kusomewa kesi yao, mahakama iliwapa masharti ya dhamana ambapo kila mshtakiwa alipaswa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwa mwajiri wao au mtendaji kata ikiwa na muhuri wa Mkurugenzi wa Manispaa.

Pia mahakama imewataka wadhamini kusaini fungu la dhamana la Sh. milioni 10 kila mmoja na hawataruhusiwa kusafiri nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.

Mapema leo Desemba 6, 2024 Watuhumiwa sita Fredrick Nsato (21),Isaack Mwaifuani(29), Benk Mwakalebela(40), Bato Twelve(32),Nelson Msela(24) na Anitha Temba(27) wamefikishwa katika Mahakama Hakimu Mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni kwa kosa la kufanya jaribio la kumteka Tarimo.

Imedaiwa, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemalila kuwa, Novemba 11 mwaka 2924, huko maeneo ya Kiluvya madukani Lingwenye , Wilaya ya Kinondoni , Dar es Salaam washtakiwa walimjaribu kumteka nyara mtu aitwaye Deogratius Tarimo kwa lengo la kumuweka kizuizini.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande hadi Septemba 19, mwaka huu kesi hiyo itakapukuja kwa ajili ya kutajwa.

Kwa mujibu upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali John Mwakifuna umedai upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...