-Waipongeza Serikali kwa kuja na mpango huo

Wananchi wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa mradi wa usambazaji na uuzwaji wa majiko ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50%

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti katika Kata ya Maji ya Chai Wilayani Arumeru Desemba 4,2024 wakati wa zoezi la uuzaji wa majiko hayo wilayani hapo.

"Tunaipongeza Serikali kwa kuja na mpango huu; ambao unakwenda kutupunguzia madhara yanayosababishwa na matumizi ya kuni kupikia," amesema Joan Palangyo mkazi wa Kata ya Maji ya Chai.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa kusambaza majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita kote nchini ikiwa ni hatua ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao umelenga ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wameachana na matumizi ya nishati isiyo safi na salama.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...