Miongoni mwa mambo waliyojadiliana katika kikao hicho ni pamoja na dhana ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha uendelezaji wa wataalam katika ngazi ya bingwa na ubingwa bobezi na kufungua fursa za wataalam wa afya kupata ajira nje ya nchi.
"Vilevile tumejadiliana kuhusu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na dawa, kuimarisha huduma za mkoba nchini kwa kufanya kambi mbalimbali za huduma za kibingwa kwa kutumia madaktari kutoka Uingereza na maeneo mengine," amesema Waziri Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa wana Diaspora hao kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...