Na Khadija Kalili Michuzi Tv.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe amezindua Wiki ya Sheria na kupokea maandamano kwenye Viwanja vya Chanzige.

Ameyasema hayo Januari 24 2025 wakati akizindua Wiki ya Sheria kwa Wilaya ya Kisarawe ambapo ameitaka Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe kuendelea kuwasikiliza wananchi kwa ukaribu ili kuondoa kero zao ili kila mmoja apate haki zake na kuendelea kupeleka kesi kwa haraka.

Aidha dkt.Jafo amempongeza Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Emmy Amon Nsangalufu kwa kuendesha kesi mbalimbali zenye malalamiko wilayani humo na kutambua mchango wake wa kutatua mashauri mbalimbali ya wananchi.

Vilevile Dkt. Jafo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe.Petro Magoti na kusema kuwa ni kiongozi wa mfano nchini Tanzania kutokana na umahiri wake wa kuwatumikia na kuwafikia wananchi na kutumia Ofisi yake kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Wakati huohuo Dkt. Jafo amewasisitiza wananchi wa Kisarawe kushiriki kwenye elimu ya Sheria watakayoipata na kuhakikisha kila mmoja anamlinda mwenzake katika masuala ya haki na usawa.

Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Kisarawe Emmy Amon Nsangalufu amesema kuwa kila mwaka Mahakama ya Tanzania imeweka utaratibu wa kuadhimisha Wiki ya Sheria ambayo kila mwanamchi atambue kuwa ni jukumu la Mahakama kuhakikisha inawafikia wananchi kwa wakati pale inapobidi na kuongeza kuwa Katika wiki hiyo wanahakikisha wanatoa elimu ya sheria kwa Wananchi itakayosababisha kupata haki zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...