Wakati vituo vya data vikitarajiwa kuchangia asilimia 20 ya matumizi ya nishati duniani ifikapo mwaka 2050, je, Afrika Mashariki iko kileleni kuwa yenye thamani ikikimbiliwa na mataifa mbalimbali duniani huku ikionyesha utajiri wa biashara zenye faida na fursa isiyo na kifani kwa nishati?

Arusha. Mnamo mwaka wa 2024, kufuatia Mkutano wa Powering Africa wa EnergyNet huko Washington DC, USA, Mara Holdings iliadhimia nia yake ya kuwekeza Afrika Mashariki kwa kutia saini makubaliano makubwa na serikali ya Kenya, kuonyesha mwelekeo wa kile ambacho kinaweza kubadilisha mwenendo kwa eneo na uhalali wa kibiashara kwa Wazalishaji Nishati Binafsi (IPP) wengi.

Katika Mkutano wa Ushirikiano wa Nishati wa Afrika Mashariki (EA-ECS), unaofanyika Januari 29-30 jijini Arusha, Tanzania, tunafuraha kuwaunganisha Wazalishaji Nishati Binafsi wa nishati za Afrika na wadau wa Uhandisi, Manunuzi, Ujenzi, na Fedha (EPCF) kutathimini uwezekano wa uwekezaji na uvumbuzi ulioanzishwa na makampuni muhimu kimkakati, ikijumuisha Vituo vya Data vya Afrika na iXAfrica.

Kiini cha ukuaji huu wa kikanda wa shughuli za uwekezaji ni Sekretarieti ya Afrika Mashariki (EAC), ambayo inawakutanisha wawekezaji na watengeneza sera pamoja na EnergyNet, kujikita katika "Utajiri wa Rasilimali. Upatikanaji wa Nishati. Fursa za Uwekezaji."

Kwa kuzingatia mafanikio ya mwaka jana, mkutano huu utakuza ushirikiano kote Afrika Mashariki, ukiangazia dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya ushirikiano wa kina wa kikanda na jukumu muhimu la kukuza viwanda na ushirikiano miongoni mwa wadau.

· Simulizi za mafanikio yaliyopatikana, ikiwa ni pamoja na njia kuu ya umeme ya Ethiopia-Kenya, inasisitiza uwezekano wa mageuzi wa ushirikiano wa kuvuka mpaka kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

· Watumiaji wa nje wanaongeza hitaji la uzalishaji wa nishati na mkutano huu utazingatia sekta ya madini na miundombinu ya kidijitali.


Ukiongozwa na Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki na watumiaji wakubwa wa nishati, kwa muda wa siku mbili, Mkutano wa Arusha utajikita katika fursa kwa sekta binafsi, kuhimiza kuwepo kwa mseto wa nishati mbalimbali ili kudumisha ustahimilivu wa gridi ya taifa ili kusaidia ukuaji mkubwa wa viwanda, pamoja na uzalishaji wa umeme kwa matumizi ya kibiashara na biashara za viwandani.

“Nishati ni nguzo ya maendeleo na ukuaji na ni muhimu kwa utendaji kazi wa uchumi wa Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki. Mkutano wa Ushirikiano wa Nishati wa Afrika Mashariki utatumika kama jukwaa bora la kuendeleza miradi na kuleta mabadiliko yanayoonekana katika sekta hiyo,” amesema Mheshimiwa Andrea Malueth, Naibu Katibu Mkuu (Sekta ya Miundombinu, Uzalishaji, Jamii na Siasa), Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

EA-ECS itakaribisha wanasiasa na viongozi mashuhuri kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na sekta zake za nishati. Wataungana na wakuzaji biashara wa sekta binafsi ambao wanatengeneza mustakabali wa mazingira ya nishati ya Afrika Mashariki, wakihudumia takriban watu milioni 500.

"Miaka kumi kutoka sasa, tabaka la kati la watu wa Afrika Mashariki litakuwa na uthabiti zaidi wa kazi, fursa zaidi, na kipato zaidi ukilinganisha na hapo awali. Reli mpya, viwanda, bandari na utalii vitalifanya eneo hili kuwa kivutio kikuu cha uwekezaji duniani, na kujitwalia nafasi hiyo kutoka eneo la Asia na Amerika Kusini," amesema Elisa Palmioli, Mtayarishaji, EnergyNet.

About EnergyNet:
FACILITATING ENERGY INVESTMENT IN FAST-GROWING ECONOMIES - EnergyNet has produced investment forums and executive dialogues for Africa and Latin America's power sectors for the last 25 years - in Europe, the USA, Asia and across Africa and Latin America.

We work with governments and national utilities to facilitate investment summits where credible international investors can build relationships with public sector stakeholders to advance access to power.

Best known for the Africa Energy Forum, the longest-serving business development meeting place for senior-level decision makers in Africa's power sector, other leading investment summits that provide strategic perspectives on the investment landscape and project preparation include the Tanzania Energy Cooperation Summit, East Africa Energy Cooperation Summit, West Africa Energy Cooperation Summit, H2 Africa, Offshore Technology Africa, Powering Africa Summit, Latin American Energy Forum and Latin American & Caribbean Gas Conference and Exhibition. YES! Youth Energy Summit and YES! Youth Energy Day are part of the portfolio, with a focus on creating a platform and network to boost the skills, connections and business readiness of a new generation of African energy leaders.

Having this focus on public and private sector partnerships provides us with a valuable lens through which we can offer independent perspectives and support the business development activities of companies from around the world operating in these fast-growing markets.

Headquarters: London, UK

For further information, please visit our website https://EnergyNet.co.UK/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...