Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi. Flora Alphonce, ametembelea banda la TCAA katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Nyamanzi kuanzia Januari 1 hadi 15, 2025.

Akiwa katika banda hilo, Bi. Flora aliungana na timu ya maonesho kutoa elimu kwa wananchi waliofika kujifunza na kupata taarifa kuhusu sekta ya usafiri wa anga nchini.

Bi. Flora alisisitiza dhamira ya TCAA katika kutoa huduma bora kwenye sekta ya usafiri wa anga, akisema, "TCAA imejidhatiti kuhakikisha inatoa huduma bora na salama katika sekta ya usafiri wa anga nchini, ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii."

Maonesho haya yanatoa fursa kwa wananchi kuelewa zaidi kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na TCAA, pamoja na mchango wake katika kuhakikisha usalama na ufanisi wa usafiri wa anga nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi. Flora Alphonce akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la TCAA kwenye maonesho ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Nyamanzi
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...