Na Mwandishi Wetu
OFISI ya Diwani Kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam imetoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani sambamba na kukata keki kwa ajili ya kusherehekea Happy Birthday ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Usomwaji wa taarifa hiyo ya utekelezaji wa Ilani pamoja na kukata keki ya Rais umefanyika leo Januari 26,2025 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Abbas Mtemvu.
Wengine waliohudhuria ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Alhaji Said Sidde pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa na Naibu Spika Wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu pamoja na Wajumbe wa NEC Mkoa akiwemo Juma
Gafafi.
Katika usomaji wa utekelezaji wa
Ilani ofisi ya Diwani Kata ya Kivukoni ambayo Diwani wake ni Sharik
Choughule imejivunia utekelezaji wa Ilani kwani kuna miradi mingi ya
maendeleo imefanya na kutumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dk.Samia kwa
kuhakikisha anasimama imara oufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
Mkuu 2020-2025.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...