Askari wanaofanya kazi kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Songwe wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kusimamia sheria za usalama barabarani kwa lengo la wananchi kuendelea kuwa na imani na Jeshi la Polisi hususani katika kikosi hicho.

Hayo yalisemwa Januari 14, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga alipokuwa akiwapongeza askari wa kikosi hicho kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya ndani ya Mkoa wa Songwe.

"Moja kati ya maadili ya Jeshi la Polisi ni kufanya kazi kwa kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa mteja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri wakati mnapowahudumia wateja huko barabarani bila kusahau kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kujiepusha na madhara yanayoweza kuepukika" alisema Kamanda Senga.

Naye, Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Akama Shaaban amesema kuwa, rushwa ni kitendo ambacho kinalitia doa Jeshi la Polisi na kulichafua Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kuondoa imani ya wananchi kwa Jeshi hilo hivyo aliwataka askari hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kueoukana nayo kabisa ili kuendelea kutengeneza taswira nzuri ya Jeshi la Polisi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...