Na Mwandishi Wetu,Unguja
MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Shadrack Mziray amewataka walengwa wa mfuko huo kutumia fedha za ruzuku vizuri kwani mpango huo awamu ya pili unatarajia kufika kikomo Septemba mwaka huu.
Ameeleza hayo katika ziara maalumu ya wadau wa maendeleo walipotembelea Shehia ya Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
“Tunawaomba mzitumie fedha hizi vizuri kwasababu mpango huu unafika kikomo Septemba, pamoja na kwamba serikali zimeshasema mpango utaendelea lakini ukifika muda huo kwanza tutawaondoa wote na kufanya utambuzi upya,” amesema
Amesema muhimu zaidi waliomo kwenye mpango kwa kipindi kilichobaki, wajidhatiti kama walikuwa na bidii waongeze zaidi ili wanachokipata kiwasaidie.
Ametumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi hao kwa kushirikiana na Tasaf kutengeneza barabara ya kilometa 1.5.
Awali wakizungumza kuhusu barabara hiyo, wananchi wa shehia hiyo wamesema awali walikuwa wakipata changamoto kubwa kwani ilikuwa haipitiki hivyo wakaipongeza Tasaf kuwaletea mabadiliko ya barabara hiyo.
Mboja Suleiman Juma amesema “tulikuwa tuna shida sana kwenda kuchota maji na watoto mgongoni tunatambaa kwani ilikuwa haipitiki hata kumpitisha mgonjwa ilikuwa tabu.”
Mwingine Miza Juma Faki amesema walikuwa na shida kubwa sana lakini wanashukuru Tasaf mpaka wamefika hatua hiyo kulikuwa na mabonde wanatambaa kupita kwenye njia hiyo.
Miongoni mwa wasimamizi wa mradi huo, Hassan Fikirini Muvura amesema wamepitia changamoto wakati wanatengeneza njia hiyo lakini wamefanikiwa.
“Njia ilikuwa haipitiki watu walikuwa wanaporomoka, wanatambaa, tunashukuru, nguvu zetu zilipotea lakini tumeona manufaa,” amesema
Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Fukuchani, Haji Muhamed Juma amesema shehia yake ina wakazi 2360 na kwamba wananchi walipata muamko wenyewe kutokana na adha walizokuwa wakizipitia kukosa njia ya Mvule.
Kutokana na changamoto hiz walipendekeza wao tukachagua wasimamizi, kwahiyo mpaka sasa wananchi tunashukuru sana,” amesema
Katika hatua nyingine Zainab Msabaha Omar ameeleza jinsi alivyotumia fedha za ruzuku kufuga kuku na kununua cherehani kwa ajili ya kushona.
Amesema baada ya kupata fedha ya mradi aliongeza madema yakafika nane kwahiyo akaendesha biashara zake na kuuza samaki.
“Nikiuza nikipata fedha nyingine naweka, nikanunua jola nikaendelea kudarizi, maisha yangu si haba tulikuwa tunaishi maisha duni lakini kwasasa alihamdulilah naendelea kufanya vyema,” amesema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...