Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella amewataka wanachama wa CCM Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza tarehe 28 Januari 2025 mkoani humo.

Mongella ametoa rai hiyo wakati akihutubia viongozi wa matawi na mashina wa Jimbo la Mchinga, Mkoa wa Lindi, leo tarehe 25 Januari 2025.

Mongella alisema CCM kinawatambua na kuwathamini viongozi hao, ndiyo maana kimeamua kufanya mapitio ya Katiba ili mabalozi waweze kushiriki katika vikao vya maamuzi.

Mkutano huo ulienda sambamba na mafunzo maalum yaliyotolewa na maafisa kutoka CCM Makao Makuu kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...