NA FARIDA MANGUBE – MOROGORO

Chuo Kikuu Mzumbe kimewatoa hofu wanafunzi ambao hawajafanya usajili chuoni hapo kwamba zoezi la usajili bado linaendelea mpaka January 10, 2025 na wapuuze taarifa zinazosambaa mtandaoni.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, akizungumza na waandishi wa habari amekanusha taarifa zilizopo kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanafunzi wanaotakiwa kuendelea na usajili ni wale tu wanapata mkopo kutoka serikalini.

Amesema kuwa taarifa hizo zimesababisha mkanganyiko mkubwa kwa baadhi ya wanafunzi na kwamba barua hiyo inayosambaa mtandaoni ipuuzwe. “Taarifa hizi hazina ukweli wowote. Menejimenti ya chuo iliamua kuongeza muda wa usajili kwa wanafunzi wote bila ubaguzi,” alisema Prof. Mwegoha.

Ametoa ufafanuzi huo baada ya kuzuka kwa taarifa potofu kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa muda wa kujisajili umeongezwa hadi Januari 10, 2025, kwa wanafunzi wenye sifa za kupata mikopo ya serikali pekee.

Kwa mujibu wa Prof. Mwegoha, tayari wanafunzi 900 kati ya 1,636 wamejisajili tangu muda wa usajili ulipoongezwa huku akitoa wito kwa wanafunzi waliobaki kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa usajili kabla ya muda kufikia kikomo.

Chuo Kikuu Mzumbe kimeendelea kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wanafunzi kufuata taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa chuo ili kuepuka taharuki zinazotokana na uvumi usio sahihi.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...