Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kabla ya kuanza kwa Mkutano wao wa Dharura uliofanyika katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC tarehe 31 Januari, 2025.

Matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa (SADC) uliofanyika katika ukumbi wa New Parliament Building, Harare nchini Zimbabwe tarehe 31 Januari, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili hali ya Ulinzi na Usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...