Na Jane Edward, Monduli

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetoa sh.Bilioni 14.4 kwa ajili ya utelelezaji wa mradi wa ulipaji fidia katika  Mradi wa Magadi Soda eneo la Engaruka uliopo Wilayani Monduli Mkoani Arusha. 

Akizungumza wakati wa akimuwakilisha Rais Samia  kwenye zoezi la uzinduzi wa ulipaji fidia hilo leo,Waziri wa viwanda na Biashara dkt. Suleiman Jafo amesema fedha hizo zimetolewa na Rais Samia ikiwa ni Mkakati wa kuendeleza miradi yenye tija kwa Taifa.

Aidha  amesema wananchi 599  kutoka vijiji vinne vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni watanufaika na fidia ya shilingi bilioni 6.2,huku fedha zingine zilizobaki zikienda katika shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.

Amesema awali mradi huo ulikwama kutokana na changamoto za kimazingira katika Ziwa Natroni na siasa nyingi zilichelewesha mradi huo lakini serikali ikafanya utafiti tena na kuja na maamuzi kutoka kwa wataalam na kuona eneo la vijiji vinne linafaa sana katika uchimbaji magadi hayo ambalo ni eneo la uwanda wa juu wa ziwa hilo lenye magadi soda ya kutosha

"Mradi huu wa magadi soda unaenda kuanza na mmepewa fidia hii kwaaajili ya kuanza mradi wake na sh, bilioni 6.2 zinalipwa ili mradi uanze na sasa hivi zabuni zimeshatangazwa na tayari wawekezaji wameanza kuonyesha nia"Alisema

Akielezea faida za mradi huo Jaffo amesema, viwanda mbalimbali vinatumia magadi soda hayo na Tanzania ni waagizaji wakubwa  wa magadi soda hayo kutoka nchi za Botswana na maeneo mengine huku ikitumia fedha nyingi za kigeni kuagiza,  hivyo mradi huo unaenda kuhamisha fedha hizo badala ya kununua nje magadi hayo yatatokea eneo la Engaruka hapa hapa Tanzania. 

"Makampuni mengi yameomba kuwekeza katika mradi huu ambao utatoa ajira hivyo nawaomba wana Longido na Monduli wajiandae kupata ajira mbalimbali"

Alisisitiza wananchi hao kujenga hoteli na nyumba bora zijengwe ili iwe fursa kubwa  ikiwemo uchomaji nyama bora ili wawekezaji waje kula nyama wakiwemo mamantilie na fursa nyingine za ajira. 

"Fedha zimeshaingizwa kwaaajili ya ulipaji fidia kupitia akaunti ya NDC huku fedha nyingine zitalipa fidia huku zilizobaki zitatengeneza miundombinu ya barabara, kituo cha afya na huduma nyingine za kijamii "Alisema

Alisema Januri hii kiongozi mkubwa atafika eneo hilo la vijiji vinne kwaaajili ya kuzindua ulipwaji wa fidia kwa wananchi hao 

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi , Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) , Dk, Nicolaus Shombe amesema mradi huo wa magadi soda umechukua miaka 29 tangu ulipoanza mchakato wake na unahistoria kubwa kwani ulianza miaka kadhaa iliyopita lakini kunamambo ya kisiasa yaliingia na kupelekea kuchelewa kuanza. 

Amesema NDC walifanya utafiti na mwaka 2010/13 kiasi cha magadi mita za ujazo bilioni 3.8 sawa na tani milioni 787 huku mahitaji ya soko yalikuwa ni tani milioni 1 kwa mwaka hivyo na eneo hilo likiwa na ukubwa wa ekari 60,884.

Ameongeza kuwa mradi huo ni zaidi ya mradi wa kimkakati na ni wa kielelezo na uta kuwa wenye manufaa makubwa katika viwanda vya vinywaji, vioo, sabuni, nguo, rangi ikiwemo viwandani.

"Baraka hii imepatikana Tanzania kwa kiwango kikubwa huku mradi huu ukinufaisha wananchi ikiwemo kupata kichocheo cha maendeleo na wiki ijayo benki mbalimbali zinatoa elimu kwa wananchi wanaopewa fidia juu ya mradi huo"Alisema

 Fredrick Lowassa ni Mbunge wa jimbo la Monduli ambapo anasema ni miaka 20 sasa wananchi waliambiwa wahame ili kupisha mradi huo na kuongeza kuwa wilaya hiyo itamkumbuka Rais Samia Suluhu Hassan kwa ulipaji fidia ili kiwanda hicho kuanza. 

Aliwashukuru viongozi wa mila (malaigwanan)kwa kufanya kazi kubwa kutuliza amani na kusisitiza fidia hiyo ya sh, bilioni 6.2 kutoka vijiji vinne kwa watu zaidi ya wananchi 595 wanapokea fedha hiyo na kusisitiza fedha hizo zitunzwe kwa kila familia na kuwasihi wananchi hao kuwekeza vitu vya maendeleo katika eneo hilo. 

Pia aliomba njia ya Monduli Juu itengenezwe ili kurahisisha usafiri na sehemu ambalo bomba linapita chini eneo lingine la juu wananchi hao waruhusiwe kulisha mifugo yao

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Frank Mbando alisema madini hayo yakichimbwa yatatengeneza bidhaa mbalimbali na hatimaye eneo hilo la Engaruka litabadilika kiuchumi kutokana na uwepo wa madini hayo katika eneo hilo. 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...