Rais wa Moët Hennessy kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, Thomas Mulliez akizungumza jijini Dar es Salaam Januari 15, 2025 mara baada ya kuwasili nchini kwaajili ya kukuza chapa ya Moët Hennessy hapa nchini. Kushoto ni Msambazaji Mkuu wa Moët Hennessy nchini Tanzania, Rajesh Davda.


Kulia ni Rais wa Moët Hennessy kwa Ulaya na Afrika, David White akizungumza jijini Dar es Salaam Januari 15, 2025 wakati wa kutangaza chapa ya Moet Hennessy nchi Tanzania katikati ni Rais wa Moët Hennessy kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, Thomas Mulliez Kushoto ni Msambazaji Mkuu wa Moët Hennessy nchini Tanzania, Rajesh Da






KATIKA kuendelea uimarisha kampuni ya Moët Hennessy kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika rais wake, Thomas Mulliez yupo nchini kwaajili ya kuonesha uwepo wa kampuni hiyo kiuchumi na kitamaduni.

Akizungumza wakati ziara hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Januari 15, 2025. Amesema amekuja kutilia mkazo na imani ya chapa hiyo ya kifahari duniani nchini Tanzania ambapo chapa yake inakuwa kwa kasi katika masoko duniani kote.

"Tanzania imekuwa mojawapo ya sehemu za uwekezaji wenye mvuto mkubwa zaidi Afrika Mashariki, ikiwa na mazingira ya kisiasa ya utulivu, mageuzi ya biashara ya kisasa, na uchumi unaotarajiwa kukua kwa asilimia 5.7% mwaka 2025, kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Moët Hennessy imekuwa sehemu inayochagiza maisha ya kifahari nchini, ikileta bidhaa kama Moët & Chandon na Hennessy kwa wateja mbalimbali na kuchangia katika maendeleo ya Ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam na kuwa kituo kikubwa cha burudani nchini Tanzania." Amesema Mulliez

Ameeleza kuwa 2024, Moët Hennessy ilionesha sura mpya katika operesheni zake hapa nchini kupitia ushirikiano na Mohan’s Oysterbay Drinks Limited (MODL), ambao ni wasambazaji maarufu wa ndani mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40.

Mulliez amesema kuwa ushirikiano huo utaongeza wigo wa soko wa Moët Hennessy na kuboresha uwezo wa usafirishaji na kuimarisha nafasi ya kampuni kama kichocheo cha nguvu za kiuchumi hapa nchini.

Ameeleza kuwa Kutokana na uwepo wa ushirikiano huo umeongeza ajira kwa kusaidia wasambazaji wa ndani, na kukuza kubadilishana uzoefu kati yao.

"Ushirikiano huu ni uthibitisho wa kujitolea kwa chapa hii maarufu katika ukuaji wa soko la Tanzania kuwa zaidi ya biashara.

Pia Mulliez ameeleza kuwa Moët Hennessy ina nia kubwa ya kushirikiana na jamii na kusherehekea Vipaji vya Kitanzania. Kupitia mpango wa Hennessy Cypher 2024, imeweka jukwaa kwa wasanii wa hip-hop wa Afrika kuonyesha ubunifu wao na kufikia watazamaji wa kimataifa.

Miongoni mwao, msanii wa Kitanzania Young Lunya alishiriki katika jukwaa ili kuchagiza ushawishi wa sanaa yake kimataifa, Juma Jux naye alikuwa miongoni mwao akionyesha ushirikiano kati ya Hennessy na tamaduni za Afrika, akionesha ubora wa Kitanzania kwenye jukwaa la kimataifa.

"Kupitia ushirikiano wake na Hennessy, Juma Jux ameudhuria matukio muhimu kama Michezo ya NBA nchini Ufaransa mwaka 2023 na Ligi ya Basketball ya Afrika ya Rwanda mwaka 2024, akiangazia uhusiano mkubwa wa Hennessy na michezo na tamaduni za Afrika." Ameeleza

Moët Hennessy pia ina ushirikiano na wabunifu maarufu wa ndani kama mbunifu Mtani Bespoke na mjasiriamali Nancy Sumari, ambao wanaonyesha ubunifu na ufanisi wa tamaduni za Kitanzania.

Mullezi ameeleza kuwa ushirikiano huo unaimarisha kujitolea kwa kampuni ya kuimarisha vipaji vya ndani na kutangaza tamaduni za Kitanzania duniani.

Ziara ya Thomas Mulliez imekuja kimkakati huku ikiweka bayana malengo na maono ya Moët Hennessy kwa soko la Tanzania. Kwa kutumia utaalamu wake wa kimataifa na kushirikiana na wadau wa ndani, kampuni ikitarajia kutoa huduma bora huku ikichangia katika uchumi na kulinda Tamaduni za Kitanzania, wakati Tanzania inajiandaa kwa ukuaji wa kiuchumi na kutambulika duniani, Moët Hennessy iko tayari kuimarisha uhusiano wake sokoni kuchagiza ukuaji lakini pia imejizatiti kuanzisha ushirikiano wa kibunifu, na kudumisha nafasi yake kama mdau muhimu katika kuchagiza uwepo wa maisha ya kifahari nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...