Na Nihifadhi Abdulla, Zanziba
TUKIWA tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 Jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ambazo zinalenga wanawake kupata uongozi kwa kuzingatia usawa wa kijinsi na kuhakikisha   50 kwa 50 inafikiwa kwenye nafasi hizo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi  haki za wanawake za kushiriki katika uongozi, ibara ya 21 inasisitiza kuwa kila raia wa Jamhuri ya Muungano ana haki sawa za kushiriki katika uongozi wa nchi aidha moja kwa moja au kwa  njia ya uwakilishi.
Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Tanzania imeridhia  mpango wa utekelezaji wa B.eijing katika maelezo ya dhamira namba 7 imeeleza uezeshaji wa mwanamke na ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa kuangalia uwiano wa jinsia ili kuhakikisha wanawake na wanaume wanapata nafasi sawa ya kushiriki katika ngazi zote za maamuzi
Licha ya hayo yote ambayo yanayompa nafasi mwanamke kushiriki kikamilifu nafasi ya uongozi lakini kunatajwa kuwepo changamoto mbalimbali zinazomkwamisha kufikia ndoto hizozakuwa kiongozi ikiwemo suala la Rushwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan mnamo june 22 2017 kipindi alipokuwa  makamu wa Rais  wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juuwa mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam alisema “kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwani ni mbaya na limeharibu sana maisha ya watu, maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo ni lazima ikomeshwe ili jamii iishi   maisha mazuri”   Mh Samia
Rushwa hutamalaki katika maeneo mbalimbali nchini ndio maana Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ZAECA kuwekeza elimu ya rushwa kwa jamii hususan wanawake  ili kuwajengea uadilifu zaidi katika kupambania haki zao.
Mgeni Salami Suleiman Mkuu wa divisheni ya elimu kwa Umma ZAECA Amesema uwepo wa sheria mpya  namba 5 ya mwaka 2023 ni maboresho ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuhakikisha  rushwa na uhujumu uchumi haipati nafasi huku akieleza kuwa “Sheria hii imekuja wakati muafaka kwa wanawake kujisimamia na kuwa mabalozi katika kuelimisha wengine ili kuepukana na tatizo hilo” amesema Mgeni
Akizungumzia jinsi sheria   inavyomlinda mwanamke katika masuala ya  kufikia ndoto za  uongozi  amesema dhamira ya Serikali ni kufikia usawa wa kijinsia wa  asilimia 50/50 ikiwa ni kufuata sheria na mikataba mbalimbali iliyoiridhia ambayo imetoa haki kwa kila mtu kushiriki katika nafasi za uongozi.
“Katika sheria hii namba 5 ya mwaka 2023   kuna kipengele cha usiri wa taarifa mfano mwanamke amekwaza katika kufikia ndoto zake kwa namna yoyote sheria ipo  rafiki yeye kupeleka taarifa zake na haitakiwi kutoka kifungu cha 15  cha   sheria hii kinamtaka mfanyakazi wa zaeca wawe na usiri na pindi ikithibitika mahakamani mfanyakazi wa ZAECA ametoa risi  anachukuliwa hatua ya kifungo miaka mitatu hivyo wanawake pamoja na makundi mengine wawe huru kuleta taarifa”amesema Mgeni

Amesema kifungu cha 52 (1) kinaeleza mtu ambaye kwa namna yoyote atashawishi, atakubali na ataahidi au ataahidi mkufanya ngono au atamfanya mtu mwengine akubali au aahidi kufanya ngono kwa ajili ya kupata huduma au kutotoa huduma ametenda kosa huku    (2) ya kifungu hicho kinaeleza endapo ngono imefanyika kwa ajili ya mnufaika wa ngono hiyo afanye jambo ambalo lipo kinyume na sheria, adhabu yake ni kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba lakini kisichozidi miaka kumi pamoja na faini isipongua shilingi milioni kumi na tano za kitanzania lakini isiyozidi milioni ishirini za kitanzania.
“Kwa vile wahanga wakuu ni wanawake kupitia     adhabu  hizi basi iwe rahisi mwanamke  akitokezewa na tatizo hilo kufika ZAECA hatua itachukuliwa  ikitokea kilamfanya makosa hayo akafungwa miaka 7 tunaimanai vitendo hivyo vitapungua au kumaliza kabisa”amemalizia mgeni
Sheria   imekuja kuongeza nguvu na kusawazisha baadhi ya mapungufu ambayo awali yalikuwepo katika sheria   iliyopita kwani inasadikika kuwa  waathiriwa wakubwa wa rushwa iwe ya pesa, ngono au yoyoye ile ni wanawake na wengi hushindwa kukabiliana nayo na hupelekea athari mbalimbali katika maisha yao ikiwemo kutojiingiza tena kwenye kinyanganyiro cha kugombea nafasi za uongozi.
Makala hii imezungumza na mwanamke ambaye ameomba hifadhi ya jina lake anasema suala la rushwa lipo lakini waliowengi hawalizungumzi kwani wanahisi ni kujitia aibu   na kujidhalilisha  wenyewe hivyo wengine huamua kukaa kando tu na siasa.
“suala la Rushwa limenifanya hadi leo hamu ya kuwa kiongozi kunitoka  karibia miongo miwili nagombania na sikupata nafasi hiyo haikunikatisha tamaa nilijua ndio masuala ya ushindani,
“nakumbuka  kuna kipindi  cha uchaguzi nami ni mmoja ya wagombania nafasi ndani ya chama,   alikuja kiongozi wa chama  ndani ya chumba nilicholala  na akanitaka nimpe rushwa ya ngono  nitapata hiyo nafasi nilichang’anikiwa   tukapishana kauli akatoka tangu siku hiyo nikaamua tu kubaki mwanachama wa kawaida” alisema
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Dkt. Mzuri Issa Amesema wanawake na wasichana wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kufikia ndoto zao za kimaendeleo ikiwemo rushwa ya ngono na hawana pahali maalum wanapoweza kukimbilia.
“Elimu bado inahitajika na kazi ya kudhibiti vitendo vya rushwa sio ya ZAECA pekee bali inahitaji ushiriki wa kila taasisi hasa ukizingatia kuwa kinga ni bora kuliko tiba”amesema mzuri
Aidha Dkt. Mzuri anasema ”kuanzishwa kwa sheria mpya ya ZAECA kutafungua ukurasa mpya katika mapambano ya rushwa hasa ya ngono katika nafasi za kazi za kitaifa na za kisiasa na hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025’’amefafanua
Mwanachama wa ACT Waazalendo Halima Ibrahim anasema    ikiwa sheria hiyo mpya itafanyiwa kazi kwa uadilifu itatoa mwanya kwa wanawake kuhamasika kuingia kwenye uongozi “ kwani wataona sasa tumepata mtetezi zile kero tutasilisha sehemu husika na hivyo ule usawa wa kijinsia tunaoulilia tutapata mwarubaini wake,
“binafsi napongeza sana juhudi hizi na natoa wito kwa wanawake wenzangu tusivumulie haya masuala ya rushwa ndio yanakwamisha juhudi zetu pengine mtu sifa zote unazo za kuwa kiongozi lakini unakatishwa tamaa kwa kitu kidogo tu tufike sehemu husika tusizembee uongozi ni haki yetu tupinaie tuufikie usawa wa 50/50”amesema Halima.
 


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...