Na Issa Mwadangala

Askari wa kike kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Songwe waungana ili kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika Machi 2025.

Kauli hiyo imetolewa Januari 30, 2025 na Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Songwe (TPF- NET) Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban Katika mkutano na Wawakilishi wa Vyombo hivyo.

ACP Akama Alisema, wakati dunia ikiendelea kuhamasisha Usawa wa kijinsia kupitia Mpango wa Maendeleo endelevu (SDG's 2030) lengo namba 5 pamoja na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa, Wanawake wa Vyombo hivyo hawana budi kushiriki kikamilifu katika siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa 8 Machi ,Kila Mwaka duniani kote.

Katika kikao hicho alielezea umuhimu wa siku hiyo ambayo inalenga kuunga mkono harakati zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika kumuwezesha mwanamke kwenye nafasi za uongozi, uchumi na maamuzi ikiwa ni pamoja na kuambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa jamii na kutoa misaada kwa makundi maalumu.

Kikao hicho cha Maandalizi ya kuelekea siku ya maadhimisho ya kilele cha Wanawake Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa Polisi Vwawa Wilaya ya Mbozi kilishirikisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Magereza, Zimamoto na Uhamiaji.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...