KAMA ilivyo kawaida wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wameendelea na zoezi lao la kurejesha kwenye jamii ambapo safari hii wameamua kuilenga zahanati ya Alimaua na kutoa msaada wa mashuka.

Wababe wa ubashiri Tanzania, Meridianbet kama sehemu ya juhudi zake za kuchangia jamii, imeendelea kurudi kwenye jamii kwa kutoa msaada wa mashuka kwa Zahanati ya Alimaua, kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.

Msaada huu unakuja katika wakati muhimu ambapo zahanati hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa muhimu vya afya. Mashuka hayo yatasaidia katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaohudhuria zahanati hiyo, na kuboresha mazingira ya kutolea huduma za afya kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram alisema, “Tunatambua umuhimu wa huduma bora za afya, na ndio maana tumejitolea kusaidia kwa vitendo. Tunatumaini msaada huu utaleta faraja kwa wagonjwa na kuimarisha huduma katika Zahanati ya Alimaua.”

Meridianbet kila siku inazidi kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakuta wakazi mbalimbali kutoka maeneno tofauti hapa jijini Dar es salaam lakini pia ujio huo huwa ni faraja kwa wale ambao wanafikiwa.

Zahanati hiyo baada ya kupokea mashuka hayo kwanza walitoa shukrani zao za dhati kwa Meridianbet ambapo walisema kuwa wanaipongeza kampuni hiyo kubwa ya ubashiri Tanzania kwa kuwaletea msaada huo kwani utaenda kuwasaidia sana.

Vilevile Meridianbet inakuambia hivi bashiri mechi za Europa leo uweze kupiga pesa sasa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao. Jisajili hapa.

Ikumbukwe kuwa zahanati hiyo ipo mijini kabisa hivyo watu wengi huitumia hivyo Meridianbet waliona mbali sana kuwapelekea msaada huo ambao ni muhumi sana kwa kipindi hiki.

Na mwisho kabisa Meridianbet kupitia mwakilishi wa Bi Nancy Ingram, walisema kuwa wataendelea kushirikiana na jamii katika miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo sekta ya afya, elimu, na ustawi wa jamii, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...