Watumishi 91 waliopata ajira mpya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na waliohamia 11 wametakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika Hospitali hapo.

Akizungumza leo katika ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Julieth Magandi amewataka watumishi kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi ambao hufika hospitalini hapo kwa mahitaji mbalimbali.

Dkt. Magandi ameeleza kuwa kulingana na idadi kubwa ya wananchi wanaohudumiwa na Hospitali hiyo huduma bora ndio kitu pekee kinachoweza kuifanya Hospitali hiyo kuendelea kuheshimika. 

 "Tuna wateja wa ndani na wateja wa nje, huduma bora ndio kitu cha msingi kwetu" amesisitiza Dkt. Magandi.

"Tunataka kila mtu atakayekuja hapa apate huduma bora, ili hata akienda huko atangaze kuwa amehudumiwa kwa viwango stahiki." amesisitiza Dkt. Magandi.

Ameongeza kuwa Hospitali hiyo inahudumia wananchi zaidi ya 4,000 kwa siku ambao kila mmoja anahitaji huduma bora.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...