Meneja wa Benki ya Stanbic tawi la Arusha, Sabuni Hemed (kulia), akikabidhi msaada wa moja ya meza kati ya meza 20 zilizotolewa na benki hiyo kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sibusiso Foundation, Martha Lukas, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Benki ya Stanbic kurudisha kwa jamii ili kuweza kusaidia watoto wanaoishi na ulemavu wa utindio wa ubongo katika kituo hicho, waweze kupata elimu itakayowafanya kuweza kujitegemea. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha hivi karibuni Mkurugenzi wa Tasisisi ya Sibusiso Foundation, Martha Lukas akitoa shukrani kwa Benki ya Stanbic Tanzania mara baada ya kupokea  msaada  wa meza 20 Kwa ajili ya kituo hicho kinacholea watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo. Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Stanbic, tawi la Arusha, Sabuni Hemed, kituoni hapo hivi karibuni. Msaada huo ukiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo kurudisha kwa jamii utawawezesha watoto hao kuwa na mazingira mazuri ya kujisomea.Benki ya Stanbic Tanzania imekabidhi msaada wa meza 20 kwa kituo cha watoto wanaoishi na ulemavu wa mtindio wa ubongo cha Sibusiso Foundation, cha jijini Arusha hivi karibuni. Msaada huo ni sehemu ya mpango wa Benki ya Stanbic kurudisha kwa jamii na kusaidia watoto hao waweze kupata elimu itakayowafanya waweze kujitegemea. Pichani ni Meneja wa Benki ya Stanbic tawi la Arusha, Sabuni Hemed (kulia) na Mkurugenzi wa kituo hicho, Martha Lucas (wa pili kushoto), watumishi wa kituo, pamoja na wafanyakazi wa Stanbic katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...