-𝑨𝒔𝒊𝒔𝒊𝒕𝒊𝒛𝒂 𝑪𝑪𝑴 𝒏𝒊 𝒊𝒎𝒂𝒓𝒂 𝒏𝒂 𝒊𝒑𝒐 𝒕𝒂𝒚𝒂𝒓𝒊 𝒌𝒘𝒂 𝒖𝒄𝒉𝒂𝒈𝒖𝒛𝒊 𝒘𝒂𝒌𝒂𝒕𝒊 𝒘𝒐𝒘𝒐𝒕𝒆.

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo 𝐂𝐏𝐀. 𝐀𝐦𝐨𝐬 𝐌𝐚𝐤𝐚𝐥𝐥𝐚 amesema mambo yote yanayohusiana na matusi na kejeli si sehemu ya utamaduni wa chama hiko.

CPA. Makalla amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaamini katika kuelekea kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka huu wa 2025 utafanyika kwa huru na haki kwa kuwa nchi inaongozwa na misingi ya demokrasia.

Mwenezi CPA. Makalla ameyasema hayo leo tarehe 1 Februari, 2025 wakati akihitimisha ziara yake ya mikoa 6 kisiwani Zanzibar.

Kwa upande mwingine, Mwenezi Makalla amezungumzia suala la baadhi ya watu kupotosha kuwa demokrasia ya kweli ni pale chama tawala kinaposhindwa katika uchaguzi na kusema si sahihi kwakuwa ushindi hutokana na namna ambavyo chama kilichopo madarakani kinavyotekekeleza ilani yake na kupelekea kuendelea kuaminiwa na wananchi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...