Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Mohamed Nyundo amewaasa wafanyabiashara na wananchi wa Kilwa kuacha kujihusisha na biashara za magendo kwani zina athari mbaya kwa jamii na uchumi wa nchi.

Nyundo ameyasema hayo leo Februari 10, 2025 wakati alipotembelewa na Timu ya Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza zoezi la kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango wilayani hapo.

"Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu." Amesema Nyundo

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Lindi Faraji Mkikima amefafanua kuwa, TRA itaendelea kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya madhara ya biashara hiyo ili kuondoa vitendo hivyo vya watu kujihusisha na biashara za magendo.

Timu ya maafisa wanaotoa elimu ya mlango kwa mlango wilayani hapo, imefanikiwa kufanya semina ya kodi kwa wafanyabiashara ambayo imefunguliwa na Mkuu wa Wilaya wa Kilwa Kivinje na pia imewatembelea walipakodi katika maeneo yao biashara na kuwaelimisha masuala mbalimbali yanayohusu kodi na umuhimu wa kulipa kodi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...