Na Mwandishi wetu: Arusha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kuusimamia Uwekezaji wa Miradi inayotekelezwa naMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mradi wa majengo ya kitega Uchumi na Mafao House.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq amesema miradi hiyo ikiendelea kutunzwa vema itasaidia kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla

Vile vile, Wajumbe wa kamati hiyo wameshauri NSSF kuendelea kuwekeza kwenye miradi yenye tija na ambayo itasaidia kuingiza kipato serikalini.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amepongeza uongozi wa Mfuko wa NSSF kwa kutoa huduma bora kwa wanachama wa mfuko huo, pia kwa usimamizi wa miradi iliyobeba fedha za wananchama.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa NSSF, Masha Mshomba amesema jengo la kaloleni kwa mwaka wa fedha 2024/25 mfuko ulipanga kukusanya kiasi cha shilingi milioni 431.30 kama kodi kutoka kwa wapangaji ambapo hadi kufikia tarehe 31 Januari, 2025 mfuko ulifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 277 sawa na 64% ya lengo la makusanyo ya mwaka.

Katika upande wa jengo la Mafao House makusanyo na thamani ya jengo katika mwaka wa fedha 2024/2025 mfuko ulipanga kukusanya kiasi cha shilingi million 1,062 kama kodi kutoka kwa wapangaji na hadi kufikia tarehe 31,Januari 2025, mfuko umefanikiwa kukusanya shilinigi milioni 509 sawa na sasilimia 48 ya lengo la makusanyo ya mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...