Na Mwandishi Wetu

HALMASHAURI ya Wilaya ya Busokelo imefanikiwa kutoa mikopo ya asilimia 10 kama takwa la kisheria na maelekezo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. 

Akizungumza kuhusu mikopo hiyo Mkurugenzi wa  Halmashauri  hiyo Dkt.Mwinyi Omary Mwinyi amesema jumla ya Sh.milioni 177 zimetolewa kwa vikundi hivyo  Februari 6,2025 ikiwa ni awamu ya kwanza ya kutoa mikopo. 

Aidha  Dkt. Mwinyi ameeleza awamu ya pili imeanza kwa usaili wa vikundi mbalimbali kuanzia Februari 2 mpaka Februari 30 mwaka huu ambapo Sh.milioni 500 zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi vitakavyopitishwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...